Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma imeahirisha kutoa hukumu ya kesi ya rufaa iliyokatwa na Clinton Damas maarufu Nyundo na wenzake watatu hadi Oktoba 21, 2025, kutokana na sababu za dharura.
Hukumu hiyo ilikuwa imepangwa kutolewa leo Septemba 25, 2025, majira ya saa 8:00 mchana, lakini imepelekwa mbele.
Wakata rufaa hao ni aliyekuwa Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) MT.140105 Clinton Damas (Nyundo), Askari Magereza C.1693 Praygod Mushi, Nickson Jackson (Machuche) na Amin Lema (Kindamba).
Ambao wanatetewa na mawakili wa kujitegemea Godfrey Wasonga, Roberth Owino na Meshack Ngamando, huku upande wa Jamhuri ukiwakilishwa na Wakili Mkuu wa Serikali Lucy Uisso pamoja na mawakili wenzake wawili.
Ikumbukwe kuwa Septemba 30, 2024, Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma iliwahukumu Nyundo na wenzake kifungo cha maisha gerezani baada ya kuwakuta na hatia ya makosa ya kubaka kwa kikundi na kumwingilia kinyume na maumbile binti mkazi wa Yombo, Dovya, Jijini Dar es Salaam, aliyetambulishwa Mahakamani kwa jina la XY.
Post a Comment