" KAMPENI YA GESI YENTE YAPONGEZWA

KAMPENI YA GESI YENTE YAPONGEZWA

 Na Tonny Alphonce-Misalaba Media 

Kampuni ya Oryx Energies imeanza kutekeleza Kwa Vitendo jitihada za serikali katika kuhimiza matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Ili wananchi waweze kushiriki moja Kwa moja katika kampeni hiyo kamapuni ya Oryx Energies ilianzisha shindano la Gesi Yente Kwa lengo la kuhimiza wananchi waweze kununua Gesi na kuachana na matumizi ya mkaa na kuni

Akizungumza na wananchi Katibu Tawala Wilaya ya Nyamagana Thomas Salala amesema wilaya ya Nyamagana imeishaanza kuhama kutoka katika matumizi ya nishati chafu na kuelekea kwenye matumizi ya nishati safi ya kupikia 

"Mtakumbuka agizo la waziri mkuu aliagiza taasisi zote za serikali zenye watu zaidi ya 100 zihame kutoka kwenye matumizi ya Kuni na Mkaa na kuanza kutumia nishati safi ya kupikia hili tumeanza kuliteleleza"alisema Salala

Amesema wao kama wilaya wanapooana Wadau wanajitokeza kuhimiza matumizi ya nishati safi ya kupikia wanawaunga mkono Ili kufikia lengo la serikali la kuhakikisha asilimia 80 ya watanzania watumie nishati safi ya kupikia Hadi kufikia mwaka 2034

Salala amempongeza kampuni ya Oryx Energies Kwa ubunifuni wa kuja na kampeni ya Gesi Yente ambayo inawasukuma wananchi kuhamasika kununua Gesi kwaajili ya kupikia.

Kwa upande wake Meneja Mkuu wa Masoko na Mauzo Shabani Fundi amesema bado elimu inahitajika kutolewa mijini na vijijini Ili wananchi wahamasike kutumia Gesi kwaajili ya kupikia.

"Tumekuwa tukigawa mitungi ya gesi bure na Ili kuhamasisha wasikae na mitungi ya gesi bila gesi tumekuwa tutoa zawadi Mbalimbali ambazo zinapatikana katika Kila mtungi wa Gesi"alisema Fundi

Robert Alfred ambae familia yake ilijishindia Baiskeli baada ya kununua mtungi wa kilo 6 amesema wanachokifanya Oryx Energies kinawapa hamasi kubwa ya kununua Gesi mara tu inapoisha

Kampeni ya Gesi Yente 

Ilianza agosti 13,2025ikitarajiwa kufanyika maeneo Mbalimbali nchini

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

Post a Comment

Previous Post Next Post