Mafundi wa kutengeneza pikipiki katika Manispaa ya Shinyanga wamepewa elimu ya kuacha vitendo vya kuwafungia wateja wao taa zenye mwanga mkali, hatua inayolenga kuepusha ajali na madhara kwa watumiaji wengine wa barabara.Elimu hiyo imetolewa na Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Shinyanga, Sajenti David Ndimila, alipowatembelea mafundi hao katika maeneo yao ya kazi na kuzungumza nao juu ya namna wanavyoweza kusaidia kupunguza changamoto za usalama barabarani.Sajenti Ndimila amesema kuwa baadhi ya mafundi wamekuwa wakifunga taa kali kwenye pikipiki za wateja wao, jambo ambalo limekuwa kero kubwa kwa watumiaji wa vyombo vingine vya moto hasa nyakati za usiku, kwani mwanga huo mkali unaweza kumsababishia dereva mwingine kupoteza uelekeo na kusababisha ajali.Ameongeza kuwa mafundi wanapaswa kutambua nafasi yao muhimu katika usalama barabarani kwa kuhakikisha huduma wanazotoa hazileti madhara bali zinasaidia kuongeza usalama. Amewataka pia kuwa walimu na washauri kwa wateja wao ili kuepuka kuwa chanzo cha ajali zinazoweza kuepukika.Aidha, Sajenti Ndimila amesisitiza kuwa kila mmoja anayo nafasi ya kuchangia katika kupunguza ajali, hivyo mafundi wanapaswa kujisimamia na kufanya kazi zao kwa weledi na kwa kuzingatia usalama wa jamii nzima.

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Post a Comment