" SIMBA RUVUMA WACHANGIA DAMU NA KUTOA MSAADA KITUO CHA AFYA MTYANGIMBOLE MKOANI RUVUMA

SIMBA RUVUMA WACHANGIA DAMU NA KUTOA MSAADA KITUO CHA AFYA MTYANGIMBOLE MKOANI RUVUMA

Na Osama Mohamedi, Misalaba Media-Songea Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya cha Mtyangimbole kilichopo katika Halmashauri ya Madaba mkoani Ruvuma, Dkt. Amos Benard Mkinga, amepongeza hatua ya uongozi wa Tawi la Klabu ya Simba mkoa wa Ruvuma kwa kuchangia damu na kutoa misaada kwa wagonjwa waliolazwa katika kituo hicho.Akizungumza mara baada ya kukamilika kwa zoezi hilo la uchangiaji damu, Dkt. Mkinga amesema kitendo hicho ni cha kuigwa katika jamii, kwani damu iliyotolewa inakwenda kuokoa maisha ya wagonjwa wanaohitaji, hasa akina mama wajawazito, watoto wachanga na wahanga wa ajali.> “Tukio hili linaonesha mshikamano wa kijamii na uzalendo wa hali ya juu. Wito wangu kwa taasisi nyingine na watu binafsi ni kuiga mfano huu wa Klabu ya Simba. Damu ni uhai,” alisema Dkt. Mkinga.Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Tawi la Simba Mkoa wa Ruvuma, Ndugu Mgaya, amesema lengo kuu la ujio wao katika kituo hicho ni kushiriki katika zoezi la kuchangia damu kwa kutambua umuhimu wake katika maisha ya binadamu.Aidha, alieleza kuwa mbali na uchangiaji damu, wamefika kituoni hapo kuwatembelea wagonjwa mbalimbali na kuwafariji kwa kuwapatia sabuni, miswaki na bidhaa nyingine za usafi wa mwili.> “Simba ni zaidi ya mpira. Tunaamini kuwa kusaidia jamii ni sehemu ya majukumu yetu kama wanachama wa klabu kubwa inayotambua mchango wa kila mwananchi,” alisema Mgaya.Wagonjwa waliolazwa pamoja na waangalizi wao walionekana kuguswa na tukio hilo ambapo walitoa shukrani za dhati kwa Klabu ya Simba kwa moyo wa kujitoa kusaidia wenye uhitaji.> “Tunaishukuru Simba kwa moyo huu wa upendo. Vitu walivyotuletea vitatusaidia sana wakati huu tunapohitaji msaada zaidi,” alisema mmoja wa waangalizi wa wagonjwa.Zoezi hilo la uchangiaji damu limekuwa sehemu ya kampeni ya kitaifa ya kuhamasisha uchangiaji wa damu salama nchini, huku zwlikihamasisha mshikamano na moyo wa kujitolea kwaJami

 

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

Post a Comment

Previous Post Next Post