" MAONESHO YA KEKI NA UPISHI YAWAVUTIA WANANCHI

MAONESHO YA KEKI NA UPISHI YAWAVUTIA WANANCHI

Na Mwandishi wetu, Misalaba Media

Maonesho ya keki na upishi wake yamewavutia wananchi kadhaa waliojitokeza kwenye ukumbi wa Ghandi Hall Jijini Mwanza huku vijana wengi wa kike wakielezea kutaka kujifunza utengenezaji wake ili waweze kupiga vita tatizo la ajira.

Mratibu wa maonesho hayo, Benard James alisema jana katika eneo hilo kuwa wameamua kufanya tukio hilo la kipekee hapa nchini kwa lengo la kuwafundisha vijana utengenezaji wa keki kwani hutumiwa katika matukio mengi ya sherehe kwenye jamii yetu hivyo itawapa fursa vijana wengi ya kupata mapato.

Alisema tukio hilo linaratibiwa na Kampuni ya BJ Empire limewaleta kwa pamoja wadau zaidi 100 ambao wanabadilishana maarifa ya jinsi ya kuboresha utengenezaji wa keki kwa kiwango bora zaidi.

Mmoja wa watengenezaji keki, kutoka Kampuni ya Mamy cakes, Mariam Hassan alisema anatengeneza keki ambazo watu wa rika zote wanaweza kutumia kwa kuwa hazina sukari nyingi.

Mdau mwingine wa upishi wa keki kutoka Kampuni ya Chelu Cakes Buswelu, alisema anatengeneza keki nzuri kwa watumiaji huku akifananisha na jiwe la Bismark ambalo ni nembo ya Jiji la Mwanza.

Kampuni ya Stronger PMC Mwanza ambao wanasambaza vifaa vya kutengeneza keki aina ya electrical wooven, mixers, blade slicer na cake display walisema wameamua kupunguza bei ya bidhaa zao ili kuwezesha kundi la vijana kutengeneza ajira kwa kazi hiyo.

Mmoja wa wafanyakazi wa Stronger PMC Mwanza, Afaq Zahor alisema kuwa wanawafundisha namna ya kutumia vifaa hivyo lengo likiwa kutengeneza Tanzania ya sasa inayotumia bidhaa za kupikia ambazo ni rafiki kwa mazingira.

Mkaazi wa Mwanza kutoka Buswelu, Rachel Laurence aliyekuwa amekuja kununua bidhaa hizo alisema amefurahia ladha ya keki hizo kwani hazina sukari nyingi hivyo ni nzuri kwa afya ya mtumiaji.

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

Post a Comment

Previous Post Next Post