" MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA KAWE CHAUMA AFANYA KAMPENI YA KIMKAKATI

MGOMBEA UBUNGE JIMBO LA KAWE CHAUMA AFANYA KAMPENI YA KIMKAKATI






Mgombea Ubunge wa jimbo la Kawe kupitia Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma), Dorcas Francis ameanzisha kampeni za kimkakati ili kuhakikisha anawafikia watu wote ndani ya jimbo hilo aweze kuwaelezea sera na namna alivyojipanga kuhakikisha anawasaidia wananchi wake.

amesema mkakati huo mpya wa kampeni jimboni humo ni Tofauti na kampeni zilizozoeleka, ambapo yeye amejikita katika mbinu za kufika kila mji, kila mtaa na kila kijiwe akishawishi makundi mbalimbali ya kijamii.

Aidha Mgombea huyo ambae pia ni kijana amejikita katika sera ya uwakilishi shirikishi huku akiahidi kuanzisha kamati za kisekta zitakazokuwa zinatoa taarifa kwa makundi yao juu ya yale yanayoendelea kuhusu idara zao serikalini naye akiyafikisha bungeni kwa ajili ya utatuzi.

“Endapo mtanichagua nitahakikisha ninaanzisha kamati maalum za kisekta zitakazokuwa zinatoa taarifa kwa makundi yenu kuhusu yale yanayoendelea kuhusu idara zenu namimi nitayafikisha bungeni kwa ajili ya utatuzi”,Amesema Dorcas.

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA




Post a Comment

Previous Post Next Post