Mjasiriamali anayejihusisha na utengenezaji wa keki Jijini Mwanza, Mariam Hassan, ameibua ubunifu wa kipekee kwa kutengeneza keki maalum yenye ujumbe wa kuhamasisha wananchi kujitokeza kupiga kura ifikapo Oktoba 29, mwaka huu.
Keki hiyo imeandikwa maneno “Kura Yako, Sauti Yako”, ikiwa na lengo la kuwakumbusha wananchi umuhimu wa kushiriki katika uchaguzi.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mariam alisema ameamua kutumia ujuzi wake katika kutengeneza keki kama njia ya ubunifu ya kuhamasisha jamii kushiriki mchakato wa kidemokrasia.
“Nimetengeneza keki hii ili kuhamasisha wananchi wajitokeze kwa wingi kupiga kura na kumchagua kiongozi ambaye ameonesha mfano wa kuleta maendeleo kwa taifa letu,” alisema Mariam.
Aidha, Mariam alibainisha kuwa keki hiyo inaweza kuliwa na watu wa rika zote kwani haina sukari nyingi, jambo linaloifanya kuwa rafiki kwa afya ya mtumiaji.
“Nataka ujumbe huu ufikie kila mtu kwa njia rahisi na ya kuvutia. Keki hii ni sehemu ya kuonesha kwamba kila mmoja ana nafasi ya kuchangia katika mustakabali wa taifa letu,” aliongeza.
Wito huo unakuja wakati taifa likijiandaa kuelekea uchaguzi mkuu, ambapo wananchi wanahimizwa kutumia haki yao ya kikatiba kwa kushiriki kupiga kura.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Post a Comment