
Na Lydia Lugakila, Misalaba MediaMbeyaWaumini wa kanisa la Tanzania Assemblies Of God(TAG) forest ya kwanza mkoani Mbeya wametakiwa kuendelea kuifuata njia ya uzima ya Yesu Kristo ili kupata uzima wa milele na kufanikiwa katika maisha.Kauli hiyo imetolewa na mtumishi wa Mungu Mchungaji Jonas Simon wakati akihubili neno la Mungu kwa niaba ya Mchungaji Thobias Tambikeni ibada iliyofanyika katika Kanisa la Forest ya kwanza T.A.G Mkoani humo.Mchg Simon mwenyeji kutoka mkoani Geita amefika mkoani Mbeya akitokea Jijini Dar es ikiwa ni mara yake ya kwanza huku akiwa na shauku ya kuona watu wa Mungu wakiokoka.Akihubili neno la Mungu kupitia ujumbe usemao njia ya uzima kutoka kitabu cha Yohana 14:1. amesema kuwa waumini wanatakiwa kuziacha njia sizizofaa na kuwa kama mtu hana njia ya uzima lazima afeli hata kama umesoma na ana digrii kibao."Mtu unataka kwenda Ulaya kusoma lazima ututengeneze njia, au unataka kufungua duka pengine la Milioni kumi lazima utengeneze njia vinginevyo huwezi kufaulu" alisema Mchungaji Simon.Ameongeza kuwa ni wakati asa waumini kutengeneza njia ya kweli ambayo ni Yesu Kristo ili kuendana na matakwa ya Mungu na si vinginevyo.Amesema kuwa kuna watu leo hii ukiwaambia kuwa Yesu ni njia pekee wanakataa hivyo mtu aliyeokoka anatakiwa asishindane na watu wasioamini waliomkaata na kumuasi Mwenyezi Mungu kwani wataambukizwa roho hiyo.Mchg Simon amesema kuwa baadhi ya waumini wameishayapotea makanisa yao huku wengine wakifirisika katika biashara na wanafunzi kufeli masomo kutokana na kuwaamini waliomkataa Mungu."Kwa mtu aliyeokoka pia anatakiwa asifadhaike, wengi wameshindwa kupokea miujiza kutokana na kufadhaika" alisema mtumishi huyo.Aidha amesema kuwa amani ya ndani ndiyo njia pekee kwa mtu aliyeokoka na mtu aliyeokoka akikaa na mtu asiyeokoka anarudishwa nyuma ki imani.Hata hivyo amesema kuwa kuna watu waliookoka zaidi ya miaka mitatu lakini hawaijui njia ya kweli huku akitolea mfano wa Anania aliyeiacha njia ya uzima na kupata taabu huku akina Musa, Daniel, Stephano wakiwa wamefanikiwa kwani hawakumuacha Mungu.Aidha ameongeza kuwa wapo waliomkosoa Mungu akiwemo Samsoni hadi kudanganywa na Delila hadi Mungu kumtolea uwepo wake.Amesema kuwa waumini wanatakiwa kujiepusha na dhambi huku akieleza kuwa kwa sasa uovu umeanzia maofisi kwa wafanyakazi na waajiri wao jambo ambalo halimpendezi Mungu.Hata hivyo amesema watu wamemsaliti yesu kwa mambo madogo madogo, na kuwahimiza waumini kutokukubali mtu audharau wokovu wa mtu badala yake aangalia njia ya msalaba na kusimama kwenye njia na kumwamini mwenyezi Mungu ili kila kitu kitokeea kwa miujiza.

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Post a Comment