HomeHABARI NETO KAPALATA- NITABORESHA MIUNDOMBINU YA BARABARA NZEGA VIJIJINI Misalaba Media September 18, 2025 0 Na Lucas Raphael, Misalaba Media -TaboraMgombea ubunge kupitia chama cha mapinduzi ccm jimbo la Nzega vijijini NetoKaparata, amewaomba wananchi wa jimbo hilo kumchagua na kukichagua chama hicho katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu iliashirikiane na serikali iboreshe miundimbinu ya barabara kwenye jimbo hiloMgombea huyo alitoa kauli hiyo jana wakati wa ufunguzi wa kampeni za jimbohilo, zilizofanyika katika uwanja wa shule ya msingi Puge kata ya puge wilaya ya nzega mkoani Tabora .Akizungumza na wananchi wa jimbo hilo alisema iwapo wananchi watampa ridhaa na kuwa mwakilishi wao kwa nafasi ya ubunge atahakikisha anaisimamia serikali inaboresha miundombinu ya barabara kwa kuzipandisha hadhi kutoka kuchongwa na kuwa za changarawe na za changarawe kuwa za kiwango cha lami. Alisema, barabara ya puge kupitia Ndala ,Nkinga na Ziba atahakikisha anasimamia kwenye kipindi chake inajengwa kwa kiwango cha lami. Aidha Kaparata alisema, ataishawishi serikali Igawe eneo la hifadhi ya Ipala iliyopo katika Kata ya ugembe ili litumiwe na wananchi katika shughuli mbalimbali za kilimo kuliko ilivyo sasa ambako wanakimbizana na kufukuzana na kukamatwa.Kwa upande wao baadhi ya wananchi wa Kata ya puge ambao walifanyika kwenye uzinduzi wa kampeni hizo wakazingumzia na kusema wagombea watekeleze ahadi zao zikiwemo ya kuboresha miundombinu ya barabara katika jimbo hilo imewkuwa ni mbovu haipitiki hasa kipindi cha masika. Mwisho 🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA You Might Like View all
Post a Comment