
Chama cha ACT Wazalendo jimbo la Shinyanga Mjini kimewaomba wananchi na wapenzi wa chama hicho kuhudhuria uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mkuu utakaofanyika kesho Jumapili, Septemba 28, 2025, katika viwanja vya Ngokolo Mitumbani.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Juster Denis Selestine, uzinduzi huo utaanza saa nane mchana (8:00) na kuendelea hadi saa kumi na mbili jioni (12:00).
Uzinduzi huo utahusisha wagombea wa udiwani pamoja na mgombea wa ubunge wa jimbo hilo, Emmanuel Ntobi, ambapo wananchi na wadau mbalimbali wa maendeleo wanatarajiwa kushiriki.
Aidha, chama hicho kimewataka wananchi kuhakikisha wanajitokeza kupiga kura kwa amani na kulinda kura zao ifikapo siku ya uchaguzi.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Post a Comment