" YANGA SC YASONGA MBELE KLABU BINGWA AFRIKA

YANGA SC YASONGA MBELE KLABU BINGWA AFRIKA






Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga SC, wamefanikiwa kutinga hatua inayofuata ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League) baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Wiliete SC ya Angola, katika mchezo wa marudiano uliopigwa leo Septemba 27, 2025 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA


Katika mchezo huo, Pacome Zouzoua alifungua ukurasa wa mabao kwa Yanga dakika ya 71, bao la pili lilifungwa dakika ya 87 na Aziz Andambwile.

Kwa ushindi huo, Yanga SC wamefanikiwa kusonga mbele kwa jumla ya mabao 5-0, baada ya kushinda mchezo wa kwanza kwa mabao 3-0 wakiwa ugenini nchini Angola wiki iliyopita.

Post a Comment

Previous Post Next Post