Na Lydia Lugakila
Mbeya
Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi CCM na mgombea Urais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta Samia Suluhu Hassan amesema bado ana kiu kubwa ya kuwaletea maendeleo Watanzania hasa wananchi wa mkoa wa Mbeya katika kuwaletea maendeleo kupitia miradi mipya na kuendeleza alipofikia kwa kipindi hiki .
Dokta Samia ametoa kauli hiyo Agosti 4, 2025 katika mkutano wa kampeni za kuwania Urais wa Jamhuri y Muungano wa Tanzania uliofanyika katika Uwanja wa Ndege wa Zamani (Old Airport) mkoani Mbeya lengo likiwa ni kuwashukuru wananchi kumuamini.
Dokta Samia amesema kuwa endapo atapata nafasi ya kupeperusha bendera ya chama hicho atahakikisha anaendeleza miradi mipya na kufanya mwendelezo wa miradi iliyopo.
Amesema serikali inakwenda kutenga fedha za mfumo maalum kwa kugharamia matibabu ya vipimo muhimu vya maradhi kwa Wananchi wasiokuwa na uwezo hasa katika magonjwa ya saratani, Figo, moyo kisukari,mishipa ya fahamu kutokana na magonjwa hayo kugharamia fedha nyingi.
Rais Samia ameongeza kuwa serikali itahakikisha pia inaweka mazingira mazuri katika sekta ya afya huku akieleza kuwa ajenda kubwa kuelekea 2030 ni kufanya kilimo kukua kwa asilimia 10 kutoka asilimia 4.6 iliyopo kwa sasa.
Aidha Dokta Samia amewashukuru wananchi mkoani Mbeya kwa mapokezi na hamasa kubwa Mkutano wa kampeni za Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM)uliofanyika katika Uwanja wa Ndege wa Zamani (Old Airport) mkoani Mbeya.
Amesema kuwa wananchi hao waliojitokeza kwa wingi katika mkutano huo wameonyesha hali ya kumpa moyo na imani ya ushindi wa kishindo.
Amesema kuwa endapo akipata ridhaa ya kupeperusha bendera ya chama cha mapinduzi (CCM) atafanya yote yanayowezekana ambapo katika sekta ya kilimo Ifikapo 2030 kilimo kitakua kwa asilimia 10 kutoka asilimia 6.4 iliyopo kwa sasa ambapo pia amewashukuru wakulima wote kwa kufanya biashara ya chakula kuimarika na kuahidi kuweka kongani ya vijana ili kuwawezesha kujiajiri wenyewe.
Hata hivyo amesema atahakikisha kujenga daraja la kuvusha watu maeneo ya mwanjelwa Mkoani humo ili kuondoa adha waipatayo wananchi.
Ameomba wana Mbeya kumuunga mkono kwa kumpigia kura za kutosha ili kufanikisha kupata nafasi hiyo na kuwaongoza Watanzania.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Post a Comment