STAND UNITED KUFANYA TAMASHA LA SIKU YA WANA 'YES! YES! YES! OKTOBA 04, 2025.
Officialgamaya0
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi, Ndg. Chrispin Kakwaya akitoa taarifa kwa vyombo vya habari juu ya tamasha la Stand United Oktoba 4, 2025 litakalofanyika uwanya wa CCM Kambarage Manispaa ya Shinyanga
Na. Elias Gamaya – Shinyanga
Timu ya Stand United inatarajia kufanya Tamasha la Siku
ya Wana Oktoba 4, 2025 katika Uwanja wa CCM Kambarage, Manispaa ya
Shinyanga, ambapo mbali na burudani mbalimbali, pia kutafanyika utambulisho
wa wachezaji wapya waliounganishwa kwa ajili ya msimu mpya wa Ligi ya
Championship.
Akizungumza leo Septemba 25, 2025 na vyombo vya habari
kuhusu maandalizi ya tamasha hilo, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi, Ndg.
Chrispin Kakwaya, amesema lengo la tamasha ni kuwapa burudani mashabiki wa
timu hiyo na kuendelea kuimarisha mshikamanano wa Stand United na wapenzi wake.
“Tamasha litaanza saa 2 asubuhi hadi saa 12 jioni. Tutakuwa
na mashindano ya mbio za baiskeli kwa wanaume na wanawake, michezo ya
utangulizi ikiwemo mechi za Bajaji vs Bodaboda, Soko Kuu vs Soko la Majengo, na
dabi ya Upongoji FC dhidi ya Ibinzamata,” amesema Kakwaya.
Mbali na michezo hiyo, alisema kutakuwa na burudani kutoka kwa wasanii
mbalimbali wa Kanda ya Ziwa na Shinyanga. Kilele cha tamasha kitakuwa ni utambulisho
wa wachezaji wapya wa Stand United kisha kufuatiwa na mtanange wa kirafiki
kati ya Stand United na timu mojawapo ya Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo itatajwa
hivi karibuni.
Kwa upande wake, Msemaji wa Stand United, Ramadhan Zorro,amesema
kiingilio katika tamasha hilo kwa mzunguko sh.5,000,VIP Sh.10,000 na VVIP
watakuwa na kadi maalum huku akitamba kuwa tamasha hilo litakuwa la aina yake
tofauti na Matamasha mingine yaliyotanguliwa kutoka kwa Timu zingine, na kutoa
wito kwa wananchi waje kwa wingi kuona kikosi ambacho wamekisajiliMsemaji wa Stand United, Ramadhan Zorro akielezea kuhusu Tamasha la Siku ya Wana 'Yes! Yes! Yes!
Post a Comment