Na Lydia Lugakila, Misalaba Media Mbeya Mgombea Ubunge wa Jimbo la Uyole kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Dkt. Tulia Ackson, ameendelea na kampeni zake kwa kufanya ziara katika Kata ya Igawilo, ambako amekutana na wananchi na wafanyabiashara mbalimbali.Ziara hiyo imefanyika Oktoba 25,2025 ikiwa na lengo la kuwahamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura katika Uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika tarehe 29 Oktoba 2025.Akizungumza na wananchi wa eneo hilo, Dkt. Tulia amewasisitiza kushiriki uchaguzi kwa amani, umoja na upendo, huku akiwataka kuendelea kuipa kura ya ushindi Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuanzia ngazi ya Urais, Ubunge hadi Udiwani.Aidha, amewapongeza wakazi wa Igawilo kwa mwitikio mkubwa katika mikutano ya kampeni na kuwataka kuendeleza mshikamano huo hadi siku ya uchaguzi."Nawasihi tushiriki uchaguzi kwa amani na tujitokeze kwa wingi na tuhakikishe tunakipigia kura chama chetu CCM kwa ushindi wa kishindo,” alisema Dkt. Tulia.Ziara hiyo ni sehemu ya mwendelezo wa kampeni za Dkt. Tulia Ackson katika maeneo mbalimbali ya Jimbo la Uyole, zikiwa na lengo la kuimarisha uhusiano kati ya mgombea na wapiga kura wake pamoja na kusikiliza changamoto zinazowakabili wananchi.








Post a Comment