Tume huru ya uchaguzi(INEC) imeombwa kuharakisha utoaji wa vitambulisho kwa waandishi wa habari kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025 ili kuepuka usumbufu wa kukimbizana dakika za mwisho.
Soko amesema hayo Jijini Mwanza wakati akihojiwa na Vyombo vya habari kuelekea uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.
Soko amebainisha kuwa, waandishi wa habari wengi hadi Sasa hawajapata vitambulisho hivyo licha ya kujisajili kwenye Mfumo maalumu wa INEC kulingana na maelekezo ya Tume yaliyotolewa.
"Tunaiomba Tume itoe vitambulisho hivyo mapema kwa waandishi walioomba ili kuepuka usumbufu usio wa lazima wa dakika za mwisho, Kwa kuwa suala la uchaguzi ni suala muhimu sana hivyo linahitaji maandalizi na sio kufanya kazi kwa presha" Alisema Soko
Soko aliongeza kuwa,Vyombo vya habari vingi vimeingia kwenye Mfumo na kujaza taarifa za waandishi wao na kukamisha lakini hadi kufikia Sasa havijapata mrejesho wa namna ya kupata hivyo vitambulisho na kuacha maswali mengi kama namna gani vitapatikana? vitachukuliwa wapi?, vitapatikana kwa mfumo gani ? na masharti ya kuvichukia yakoje?
Soko ameiomba Tume kujitokeza na kutoa taarifa rasmi juu ya zoezi la utoajii wa vitambulisho au ikiwezekana wavitoe mapema ili kuondoa usumbufu.
"Nina imani Tume ina weledi mkubwa kwenye kusimamia uchaguzi hivyo nina imani ombi letu litashughulikiwa" Alisema Soko.
Ikumbukwe kuwa, kila uchaguzi mkuu kumekuwa na utaratibu wa Tume kutoa vitambulisho maalumu kwa waandishi wa habari ili waweze kutekeleza wajibu wao kisheria siku za uchaguzi mkuu, hivyo zoezi ni endelevu kwenye uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025 lakini kilio Cha waandishi wengi ni kuchelewa kutolewa kwa vitambulisho hivyo.


Post a Comment