" KIKUNDI CHA POLISI JAMII FITNESS CENTER SHINYANGA CHAZINDUA KAMPENI YA MARATHON KUCHANGIA SHILINGI MILIONI 520 KWA AJILI YA UNUNUZI WA PIKIPIKI

KIKUNDI CHA POLISI JAMII FITNESS CENTER SHINYANGA CHAZINDUA KAMPENI YA MARATHON KUCHANGIA SHILINGI MILIONI 520 KWA AJILI YA UNUNUZI WA PIKIPIKI

Kikundi cha Polisi Jamii Fitness Center cha Manispaa ya Shinyanga kimezindua rasmi kampeni ya mbio za marathon zenye umbali wa kilomita 5, 10 na 21 na vifaa mbalimbali vitakavyotumika kwa lengo la kukusanya shilingi milioni 520 kwa ajili ya ununuzi wa pikipiki zitakazotumiwa na maafisa wa Polisi Jamii katika kuimarisha utendaji wao wa kazi.Mwenyekiti wa mbio hizo za marathon, Ignas Banyema ameushukuru uongozi wa serikali ya mkoa wa Shinyanga kwa kuendelea kushirikiana nao katika kutimiza malengo yao na kuuomba uongozi wa serikali ya Mkoa kupitia ofisi ya Mkuu wa Mkoa kuwasaidia katika kutafuta wadhamini watakaosaidia kufanikisha zoezi hilo. “Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya tunakushukuru sana kwa utayari wako kufika hapa leo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wetu wa Shinyanga Mheshimiwa Mboni Mhita umeuzindua rasmi mpango wa Shinyanga Marathon pamoja na vifaa vitakavyotumika katika mbio hizi tunaomba serikali ya mkoa iendelee kutushika mkono katika hatua zote za kupata wadhamini kwani lengo letu ni kukusanya shilingi milioni 520 ili kufanikisha ununuzi wa pikipikij kwa askari wetu wa Polisi Jamii,” amesema Banyemaa.Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Wakili Julius Mtatiro amekipongeza kikundi hicho kwa ubunifu na juhudi zao na kuahidi kuwa serikali ya Mkoa itaendelea kushirikiana nao hadi malengo yao yatimie. “Serikali ya mkoa itaendelea kuwa bega kwa bega nanyi kwani malengo yenu ni mazuri na yenye manufaa makubwa kwa Polisi Jamii wetu na jamii kwa ujumla, endeleeni na jitihada hizi kwani mazoezi ni afya na pia yanaunganisha watu lakini pia niwakumbushe pia kuendelea kushiriki ipasavyo katika zoezi la uchaguzi mkuu,” amesema Mtatiro.Kikundi cha Polisi Jamii Fitness Center kimekuwepo kwa zaidi ya miaka 10, kikiwa na washiriki zaidi ya 200 huku kaulimbiu ya mwaka huu inasema “Kimbia kwa afya, imarisha usalama wa raia na mali zao.”


 

Post a Comment

Previous Post Next Post