" MATEMBEZI YA AMANI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU YAFANYIKA MKOANI MBEYA WANANCHI WAHAMASISHWA UPIGAJI KURA WA AMANI BILA VURUGU YOYOTE

MATEMBEZI YA AMANI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU YAFANYIKA MKOANI MBEYA WANANCHI WAHAMASISHWA UPIGAJI KURA WA AMANI BILA VURUGU YOYOTE

Na Lydia Lugakila, Misalaba Media Mbeya Matembezi ya amani yamefanyika  Mkoani Mbeya katika mji mdogo wa Mbalizi, lengo kuu likiwa ni kuhamasisha utulivu, mshikamano, na ushiriki wa uchaguzi kwa amani unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, mwaka huuAkizungumza katika matembezi hayo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, SACP Benjamin Kuzaga, amewataka wananchi mkoani humo kutoshiriki katika vitendo vya kuvuruga amani wakati wa Uchaguzi mkuu na kwamba jeshi hilo limejipanga kikamilifu kuhakikisha ulinzi na usalama unaimarishwa wakati wote."Tunaomba wananchi wajiepushe na vitendo vyovyote vinavyoweza kusababisha uvunjifu wa amani" alisema Kamanda kuzaga.Tushiriki uchaguzi kwa utulivu na tuweke mbele maslahi ya taifa letu,” aliongeza Kamanda Kuzaga.Tukio hilo la matembezi limeratibiwa na Ofisi ya mkurugenzi wa Halmashauri ya Mbeya.Aidha Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mbeya , Bi. Erica Yegella, amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura ili kutumia haki yao ya msingi ya kikatiba."Kila Mwananchi ana wajibu wa kushiriki uchaguzi kwa kupiga kura hivyo ni haki ya msingi ambayo inatupa nguvu ya kuchagua viongozi tunaowataka,” alisema Bi. Erica Yegella.Baadhi ya wananchi hao akiwemo Abuu mtoto na Christina Richard na watumishi wa serikali walioshiriki matembezi hayo wameeleza kuwa wapo tayari kushiriki uchaguzi huo kwa amani na kufuata sheria."Tumejiandaa kupiga kura kwa utulivu tunataka kuona mabadiliko kupitia sanduku la kura,” alisema mmoja wa wananchi waliohudhuria tukio hiloMatembezi hayo  yalihusisha watumishi wa serikali, Jeshi la Polisi, Wananchi, na Waandishi wa habari, huku yakiwa na ujumbe maalum wa kuhamasisha amani na ushiriki katika Uchaguzi huko.

Post a Comment

Previous Post Next Post