Siku ya maamuzi Oktoba 29, 2025 inakaribia ! Kura yako ni zaidi ya kupiga mstari; ndio njia kuu ya kuwasha injini ya maendeleo ya nchi. Tanzania inasonga mbele kwa kuwekeza kwenye rasilimali zetu asili – bahari, maziwa, mito, na mabwawa. Hizi si ahadi tu, ni Uchumi wa Kisasa unaokuja na ajira, biashara, na fursa nyingi kwetu sote.
Kwa chama tawala Chama cha Mapinduzi (CCM) ambacho mambo yake mengi yanakwenda yamenyooka katika Ilani ya Chama hicho cya 2025–2030 inakuja na mipango kabambe kwa vijana. Wamedhamiria kuongeza kasi ya maendeleo katika Uchumi wa Buluu. Hii inathibitishwa na miradi mikubwa inayotarajiwa kama vile ujenzi wa Bandari ya Uvuvi Bagamoyo na ukamilishaji wa Bandari ya Uvuvi Kilwa.
Hizi zitatumika kama vituo vya kuchakata na kuongeza thamani ya mazao, huku samaki wa bahari kuu wakipakiwa, kuchakatwa, na kuuzwa kimataifa. Hapa ndipo ajira mpya na utajiri kwa taifa zinapozalishwa.
Kura Ndio Kiunganishi Kati ya Ahadi na Utekelezaji
Kama ilivyokuwa enzi za Kura Tatu ambapo kura iliamua mwelekeo wa kisiasa, leo kura ndio inahakikisha miradi hii inatoka kwenye karatasi na kufika mtaani kwako.
Ikumbukwe kuwa unapopiga kura Oktoba 29, unachagua kiongozi unayemwamini atasimama imara na kuhakikisha bajeti ya miradi kama Bandari ya Bagamoyo haipotei. Kura yako ndio uhakiki (audit) wa kwanza wa kazi.
Chama Tawala (CCM) kimetoa ahadi zake. Kura yako ndio tathmini ya utendaji wao. Wametekeleza? Wapigie kura waendelee! Wamefeli? Wape kura chama kingine! Kura ndio inayomfanya kiongozi awe mwajibikaji kwako, kijana.
Kwa kupiga kura unalinda fursa ya ajira yako hasa pale ambapo bahari inakwenda kuwa chanzo cha fursa kwa kizazi kijacho. Uwekezaji katika meli za uvuvi wa bahari kuu unahitaji uongozi thabiti. Kura yako inachagua kiongozi anayelinda rasilimali hizi kwa hekima na kwa manufaa ya muda mrefu, si kwa faida ya muda mfupi.
mwisho
Post a Comment