" KURA HUCHAGIZA MAENDELEO YA TAIFA: KUTOKA AHADI HADI UTEKELEZAJI

KURA HUCHAGIZA MAENDELEO YA TAIFA: KUTOKA AHADI HADI UTEKELEZAJI

 Na Mwandishi Wetu

Kura ndio msingi wa maamuzi ya nchi, kura hutumika kuchagua chama kinachotoa ilani na viongozi wanaowajibika kuitimiza. Kura yako haichagui tu Rais au Mbunge, bali inakipa madaraka ya utekelezaji chama kinachoamini katika matumizi endelevu ya rasilimali za maji, bahari, mito, maziwa, na mabwawa.

Umuhimu wa Kura 

Kwa kuwa kura huwajibisha utekelezaji wa Ilani wananchi wanapaswa kufuatilia ilani hizo kuzielewa na kutafakari Ilani za vyama mbalimbali kabla ya kuingia katika sanduku la kura Oktoba 29.

Mathalani  Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) 2025–2030 inaahidi mambo makubwa katika Uchumi wa Buluu, kama vile ujenzi wa Bandari ya Uvuvi Bagamoyo na Kilwa, kuwezesha wavuvi kwa mikopo na vifaa vya kisasa, na kuanzisha vituo vya ukuzaji viumbe maji.

Kwa hiyo mwananchji kama ameridhika na maelezo haya maana yake kama anataka kilichozungumzwa ataipatia Kura  (idhini) Chama Tawala kutumia rasilimali za Taifa kutekeleza ahadi hizi. Bila kura yako, chama hicho hakiwi na nguvu za kisheria wala kisiasa kuendeleza meli za uvuvi wa bahari kuu au kuimarisha masoko ya samaki na mialo. Kura ndiyo njia ya kumfanya kiongozi ajisikie anafanya kazi kwa ajili ya wananchi na si kwa ajili yake binafsi.

Hivyo kura yako hutumika kutoa alama ya kupita au kufeli. Iwapo Serikali iliyopo madarakani imetekeleza miradi mikubwa kama inavyoahidi, mfano, kutoa mikopo kwa wakulima wa mwani na wavuvi au kujenga mabwawa, wananchi wanaweza kuendeleza uwepo wake kwa kuipigia kura tena.

Ikiwa utendaji hauridhishi, kura huipa nafasi chama kingine cha upinzani kuingia na kujaribu kutekeleza ilani yao. Kwa hiyo, kura ndiyo mfumo wa usimamizi (check and balance) unaodhibiti Chama Tawala; ndiyo inayoamua namna gani Chama Tawala kitaendelea kuwepo—kwa kufanya vizuri au kuondolewa kwa kutofanya vizuri.

Uchumi wa Buluu umeelezwa kama "zaidi ya mawimbi; ni dira ya uzalendo na ubunifu." Miradi kama Bandari ya Bagamoyo inataka kufanya Taifa letu kutumia rasilimali zake kwa hekima na maendeleo.

Kwa maneno mengine vijana wanapopiga kura, wanathibitisha uzalendo wao kwa kuchagua viongozi ambao wanaamini watalinda rasilimali za Taifa kwa ajili ya vizazi vijavyo. Kura yako inalinda bahari, maziwa, na mito isitumiwe vibaya, na badala yake iwe chanzo cha ajira, biashara, chakula na utajiri. Kura ndiyo inaweka ulinzi wa kidemokrasia kuhakikisha ahadi za uwekezaji katika mabwawa na vizimba vya samaki vinakuwa fursa za kibiashara na si maneno matupu.

Kwa kifupi, kura yako haiamui tu mshindi wa uchaguzi; inatoa idhini ya kutekeleza maendeleo ya Taifa na inakupa uwezo wa kuwawajibisha wale wote walioahidi kwamba Uchumi wa Buluu ni dira ya mustakabali wa Tanzania.

@@@@@@@@@@@@@@



Post a Comment

Previous Post Next Post