
Na Mwandishi wetu, Misalaba MediaDkt. Emmanuel Nchimbi, amewahakikishia wananchi wa Kilwa kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kina mipango madhubuti ya kutatua kwa kudumu tatizo la wanyama waharibifu linalowakumba wananchi wa maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo.Dkt. Nchimbi ametoa kauli hiyo wakati wa mwendelezo wa kampeni za kunadi sera za chama katika kata ya Tingi, jimbo la Kilwa Kaskazini, ambako aliwataka wananchi kumchagua mgombea wa CCM ili waweze kupata suluhisho la kudumu kwa changamoto hiyo inayowaathiri moja kwa moja katika maisha yao ya kila siku.“Chama chetu kina sera na mikakati thabiti ya kushughulikia tatizo hili la wanyama waharibifu. Tukipewa ridhaa, tutalitatua kwa njia ya kudumu ili wananchi waendelee na shughuli zao za kilimo na ufugaji bila hofu,” alisema Dkt. Nchimbi.Kwa upande wake, mgombea ubunge wa jimbo la Kilwa Kaskazini kwa tiketi ya CCM, Mhe. Kinjekitile Ngombale Mwiru, ameeleza kuwa tatizo hilo limekuwa sugu kwa wananchi kwa miaka mingi, na sasa ni wakati wa kuwaamini viongozi wa CCM ili wapate msaada wa kweli.“Wananchi wamechoshwa na wanyama wanaovamia mashamba yao, kuharibu mazao na kuhatarisha maisha yao. Tunahitaji hatua za haraka na za kudumu,” alisema Mhe. Kinjekitile.

Post a Comment