" MGOMBEA WA CHAUMA AOMBA SIKU 100 ZA KWANZA KUIBADILI NYAMAGANA.

MGOMBEA WA CHAUMA AOMBA SIKU 100 ZA KWANZA KUIBADILI NYAMAGANA.


Tonny Alphonce -Misalaba Media 

Mgombea Ubunge Jimbo la Nyamagana kupitia Chama Cha Ukombozi wa Umma(CHAUMA) Evance Mabugo ameomba siku 100 ziwe kipimo Cha  uongozi wake Kwa wananchi wa Nyamagana.

Akizungumza kuhusiana na mwenendo wa kampeni zake za kuusaka Ubunge Jimbo la Nyamagana Evance amesema kilichokosekana katika jimbo hilo ni kupata kiongozi mdadisi na mfatiliaji wa mambo yanayowagusa wananchi.

"Nyamagana tunashida ya maji Kwa muda mrefu na vyanzo vya maji vipo lakini kinachokosekana ni ufuatiliaji tu na ndio maana naomba wananyamagana wanipe siku 100 za kwanza nianze na kero hii"alisema Evence 

Kuhusiana na wakazi waishio Milimani Evance amesema endapo atachaguliwa Kuwa mbunge wa Nyamagana atahakikisha viwanja vilivyopo milimani vinapimwa na wananchi wanapatiwa Hati zao.

"Wananchi wanaoishi milimani wanahakinya kupata Hati Ili ziweze kuwasaidia kupata mikopo lakini pia kupata uhakika wa makazi Yao."alisema Evance 

Akizungumzia mwendelezo wa kampeni zake Evance amewashukuru wakazi wa Nyamagana Kwa kujitokeza katika mkutano ya kampeni ya CHAUMA na kuwaunga mkono.

Evance amewaomba wananyamagana wamwamini na wamchague Kuwa mbunge Ili aweze kuwatumikia na kutatua kero zote zilizopo katika jimbo hilo.

Post a Comment

Previous Post Next Post