" POLISI WATAHADHARISHA UWEPO WA PICHA ZA KUTENGENEZWA KULETA MIHEMKO

POLISI WATAHADHARISHA UWEPO WA PICHA ZA KUTENGENEZWA KULETA MIHEMKO


Jeshi la Polisi  limetahjadharisha wananchi kuwa, kuna kikundi cha watu baada ya kuona wameshindwa kuvuruga amani ya nchi wameunda kikundi cha vijana ambao wanaandaa picha mjongeo na taarifa mbalimbali za matukio yaliyotokea siku za nyuma ambayo Polisi waliyafanyia kazi na mengine ya kutunga ili wayasambaze kwenye mitandao ya kijamii yaonekane yametokea kipindi hiki au muda mfupi uliopita ili kuleta sintofahamu.

Pamoja na tahadhari hiyo Jeshi la Polisi limesema linaendelea kuwahakikishia wananchi kuwa kuna usalama wa kutosha tunapoelekea kesho tarehe 29.10.2025 siku ya kupiga kura, kwani hakuna tishio lolote la kiusalama kama walivyowahakikishia wananchi  kwa taarifa waliyoitoa Oktoba 26, 2025.

Akifafanua zaidi Msemaji wa Jeshi la Polisi , David Misime amewataka wananchi watambue kuwa habari hizo zitakazokuwa za uongo, uzushi ni za kutaka kuchonganisha na kugombanisha ili watimize nia yao ovu dhidi ya amani ya taifa . 

"Wapo pia walioandaliwa kama ambavyo baadhi wamesha jitokeza kuzungumza na kutoa taarifa zenye tungo tata, zenye kutaka kuleta taharuki. Pia wanakusanya matukio ambayo yaliyotokea nchi zingine na kuyatengeneza kwa kuyawekea sauti zenye tafauti ya kiswahili ili yaonekane yanatokea nchini mwetu wa kati huu muhimu tunaopelekea kupiga kura kesho," alisema Misime.

Aidha amesema jeshi hilo pia limemaizi uwapo wa mipango ya kuchukua picha za baadhi ya viongozi na kuziwekea maneno na sauti zenye matamko ya upotoshaji ili ionekane wao ndio wanazungumza au wanayatamka wakati si kweli.

Misime  amesema  wakati Jeshi la Polisi linaendelea kuwafuatilia ili wawatie nguvuni kwa mujibu wa sheria, linatoa rai kwa wananchi watakapo ona au kutumiwa picha mjongeo na taarifa kama hizo au vipeperushi na mengine yanayofanana na hayo wayapuuzie kwani yameandaliwa kwa nia ovu au kinyume na lengo la kutaka kuleta taharuki kwa wananchi.

Aidha, amesema wakitumiwa taarifa kama hizo wasisambaze kwani kufanya hivyo ni kosa la jinai kwa mujibu wa sheria ya ya makosa ya kimtandao badala yake wazifute.

 

Post a Comment

Previous Post Next Post