" Rais wa CAF Patrice Motsepe Akanusha Tetesi za Kutaka Kugombea Urais Afrika Kusini

Rais wa CAF Patrice Motsepe Akanusha Tetesi za Kutaka Kugombea Urais Afrika Kusini

 Rais wa CAF Patrice Motsepe Akanusha Tetesi za Kutaka Kugombea Urais Afrika Kusini

Rais wa CAF Patrice Motsepe Akanusha Tetesi za Kutaka Kugombea Urais Afrika Kusini

Rais wa Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF), Patrice Motsepe, amekanusha uvumi ulioenea hivi karibuni kwamba anataka kugombea Urais wa Afrika Kusini, akisema nchi hiyo haihitaji kutawaliwa na tajiri.

Inakuja baada ya ripoti mapema mwaka huu kwamba Mwanaharakati huyo, anapanga kuchukua nafasi ya Rais Cyril Ramaphosa katika Uongozi wa African National Congress (ANC) na kuwa Rais wa Afrika Kusini.

Akizungumza katika mkutano wa kila mwaka wa jukwaa la wataalamu wa Vyombo vya habari nchini Afrika Kusini (SANEF), Motsepe alisema hana ajenda ya kisiasa, licha ya baadhi ya ANC kumtaka aongoze chama.

Alisema bado yuko makini katika chama kilichoasisiwa na Nelson Mandela (ANC), lakini akasisitiza kuwa Afrika Kusini haihitaji kuwa na Rais kwani yeye ni tajiri na ofisi ya Rais inahitaji mtu mhimu zaidi.

Alisema Afrika Kusini ina watu wengine wenye sifa za uongozi.

Post a Comment

Previous Post Next Post