Taasisi ya vyombo vya habari kusini mwa Afrika (Misa Tanzania) imesisitiza maridhiano ili kuendelea kua na Tanzania bora yenye amani, mshikamano na umojaWakati tukiendelea kuwafariji watanzania wakiwemo wanahabari waliopata madhila yaliyotokana na kadhia wakati wa uchaguzi hivyo inatoa rai kwa vyama vya siasa ,taasisi za dini,vyombo vya habari ,makundi ya kijamii na wananchi kutafuta suluhu na maridhiano ya kitaifa ili kuponya majeraha Akitoa taamko hili kwa niaba ya taasisi hiyo November 7,2025 mwenyekit wa taasisi ya vyombo vya habari kusini mwa Afrika (Misa Tanzania) Edwin Soko amesema ipo haja ya kuimarisha misingi ya haki,uhuru na amani ya nchi "Ni vigumu kuamini au kuelewa matukio yaliyojiri wakati na baada ya uchaguzi mkuu wa tarehe 29 Octoba 2025 ni matukio yaliyowaumiza watanzania kihisia ,kiakili na kimwili ,kwani zipo familia zilizopoteza wapendwa wao ,zinazowaaguza majeruhi na zilizopoteza mali na biashara huku watanzania wakikosa haki ya kikatiba ya kupata taarifa kupitia vyombo vya habari na njia za mawasiliano ya kidijitali "amesema SokoAmeongeza kua kwa namna ya kipekee Misa Tanzania inaungana na watanzania wote kutoa pole kwa familia zilizopoteza wapendwa wao ,wanawaombea majeruhi wote wapate nafuu na kupona haraka, aidha miongoni mwa walioathirika ni baadhi ya waandishi wa habari hivyo wanahimiza kulindwa kwa haki ya kupata taarifa
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

Post a Comment