Na: Mbeki Mbeki.
Karagwe.
Mamilioni ya watu dunia(leo Desemba 2025) wanajiandaa kuupokei mwaka 2026 kwa Shangwe ,fataki,sala na salamu za heri .
Lakini nyuma ya sherehe hizo ,swali moja linabaki 1 januari ilitoka wapi,na nani alianzisha iwe likizo ya mapumziko .
Mageuzi ya kalenda: Historia inaonesha kuwa mwaka mpya 1 januari unamizizi yake katika dola ya Roma ya kale,kabla ya kuja kwa mfumo wa kisiasa wa kalenda ,mataifa mengi yalianza mwaka kwa kufuata majira ya kilimo,dini,au siasa.
Hata Roma ya mwanzo wa mwaka ,hadi pale Julius caesar alipoamua kuifanyia marekebisho kalenda ya Kirumi.
Mnamo mwaka 46_45 kabla ya kristo (KK) Caesar alianzisha kalenda ya Julian,na Januari 1ikatangazwa rasmi kuwa siku ya kwanza ya mwaka wa kalenda .
Hatua hiyo lilikuja kuwa rejea kubwa kwa mifumo ya kalenda duniani kwa Karne zilizofuata.
Kalenda ya Gregorian na kuenea kimataifa mwaka 1582 ,papa Gregory x111 alifanya marekebisho mapya ya kalenda ya Gregorian ,ambayo ndiyo inayo tumika zaidi duniani leo.
Marekebisho hayo yalidumisha 1 januari kama mwanzo rasmi wa mwaka wa kiraia ,nanchi nyingi ziilianza kuipokea kalenda hiyo taratibu kadri Karne zilivyosonga.
Likizo haikuanzishwa na mtu mmoja bali serikali za mataifa.
Wakati Caesar na Papa Gregory walirekebisha kalenda hawakuitangaza I januari kuwa likizo ya mapumziko rasmi( public Holiday) ulifanywa baadaye na serikali za mataifa kulingana na katiba na sheria zao.
Kwamfano:
* Japan ilianza kuitambua 1 januari kama likizo rasmi ya kitaifa mwaka 1948 ,baada ya serikali kupitisha mfumo mpya wa sikuu za umma.
* Nchi nyingi barani ulaya na kwingineko zilianza kuifanya 1januari kuwa likizo baada ya kupokea kalenda ya Gregoria na kuipa uzito wa kijamii na kimataifa katika sheria.
Tanzania kama ilivyo kwa mataifa mengine yanayotumia kalenda ya kiraia,pia huitambua 1januari kuwa likizo ya mapumziko kwa mujibu wa sheria za sikukuu za umma.
Mwaka mpya na Biblia. Ingawa sherehe za 1 januari hazikutajwa moja kwa moja kwenye Biblia ,maandiko yanatambua kuwa Mungu ndiye mwanzilishi wa majira,siku,na miaka( Mwanzo 1: 14).
Wakristo wengi leo hutumia siku hii kwa shukrani ,maombi,na kutafakari malengo ya mwaka mpya ,huku wakiepuka mambo yanayokiuka maadili ya kiimani.
Januari haikuanzishwa kuwa likizo na mtu mmoja,wala taifa moja pekee ,bali ni urithi wa mageuzi ya kalenda ya Roma,na baadaye serikali za mataifa zikaipa hadhi ya mapumziko.
Kadri dunia inavyoingia mwaka mpya kiini cha tukio hilo linabaki kuwa mwanzo mpya wa kalenda ya kiraia,nifursa ya kuimarisha umoja ,matumaini ,na shukrani kwa muumba.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment