Na Lydia Lugakila, Misalaba Media MbeyaDesemba 22, 2025, Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Mbunge wa Jimbo la Uyole, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, amewahimiza wananchi wa Jimbo la Uyole kujitolea na kusaidiana, hususan kuwajali wananchi wenye uhitaji.Dkt.Tulia ametoa wito huo wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Igawilo, katika kukabidhi vyakula kwa baadhi ya wananchi wenye uhitaji kwa ajili ya sikukuu. Amesisitiza umuhimu wa mshikamano na huruma katika jamii akisema:“Wenye uhitaji ni wengi, hivyo ni muhimu tujenge utamaduni wa kusaidia waliopo katika mazingira magumu ili wote tuweze kutabasamu.”Katika zoezi hilo, Dkt. Tulia ametoa msaada wa chakula kwa kaya zenye uhitaji ikiwa ni mwendelezo wa juhudi zake za kusaidia familia zisizojiweza ndani ya Jimbo la Uyole.Aidha jumla ya kata tano ambazo ni Ilemi, Isyesye, Itezi, Nsalaga na Igawilo zimefikiwa, na kufanya idadi ya kata 48 kufikiwa hadi sasa.Dkt. Tulia amesema zoezi hilo litaendelea katika kata nyingine zilizobaki ili kuhakikisha wananchi wote wenye uhitaji ndani ya Jimbo la Uyole wanapata msaada huo, hususan katika kipindi hiki cha sikukuu.🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254




Post a Comment