" DKT. TULIA ATOA MSAADA WA CHAKULA KWA KAYA 134 ZENYE UHITAJI ZAIDI JIMBO LA UYOLE

DKT. TULIA ATOA MSAADA WA CHAKULA KWA KAYA 134 ZENYE UHITAJI ZAIDI JIMBO LA UYOLE

Na Lydia Lugakila –Misalaba MediaMbeyaSpika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Uyole, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, Disemba 23, 2025 amehitimisha zoezi la utoaji wa msaada wa chakula kwa kaya 134 zenye uhitaji zaidi katika Jimbo la Uyole.Zoezi hilo limehusisha kaya kutoka kata zote 13 za Jimbo jipya la Uyole, likiwa na lengo la kuwasaidia wananchi wenye mazingira magumu hasa katika kipindi hiki cha sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya, ili nao waweze kusherehekea kwa furaha na matumaini kama wananchi wengine.Akizungumza na wananchi wa Jimbo la Uyole, Dkt.Tulia amesisitiza umuhimu wa kujenga utamaduni wa kusaidiana, akibainisha kuwa katika jamii zetu wahitaji ni wengi na msaada wa aina yoyote una mchango mkubwa katika kuleta faraja na tabasamu.“Katika jamii zetu wahitaji ni wengi, hivyo ni muhimu kujenga utamaduni wa kusaidia wale wenye uhitaji ili wote tuweze kutabasamu."Tusaidiane kwa kile tulichonacho, hata kama ni kidogo,” amesema Dkt. Tulia.Katika zoezi hilo, kila kaya iliyochaguliwa imekabidhiwa mchele wa kilo 20 pamoja na fedha kwa ajili ya mboga, hatua inayolenga kuhakikisha walengwa wanapata mahitaji ya msingi na kushiriki kikamilifu katika shamrashamra za sikukuu.Wananchi wa Uyole wamepongeza jitihada hizo wakizitaja kuwa ni faraja kubwa kwa familia zenye uhitaji, huku wakiahidi kuendeleza mshikamano na moyo wa kusaidiana katika jamii zao.Hatua hii ya Dkt. Tulia inaendelea kuonesha dhamira yake ya dhati ya kuwajali wananchi na kuchangia ustawi wa jamii, hususan kwa makundi yenye uhitaji maalum.

 

Post a Comment

Previous Post Next Post