Na Fabius Clavery, Misalaba Media-Kagera.
Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini mkoani Kagera, Mhandisi Johnston Mutasingwa, amewatakia wananchi wa jimbo hilo Kheri ya sikukuu za Krismasi 2025 na Mwaka Mpya 2026, huku akiwahimiza kusherehekea sikukuu hizo kwa amani, upendo na mshikamano.
Akizungumza Desemba 23, 2025, katika ofisi yake iliyopo Bukoba Mjini, Mhandisi Mutasingwa amesema wakati wa sikukuu za Christmas na mwaka mpya ni kipindi cha kudumisha amani, kuimarisha mahusiano ya kijamii na kuepuka vitendo vinavyoweza kuhatarisha usalama wa wananchi.
Aidha, mbunge huyo ametoa wito kwa wananchi kusherehekea sikukuu ya Krismasi kwa kufanya matendo ya huruma, hususan kwa watu binafsi na makundi yenye mahitaji maalum, ikiwa ni pamoja na watoto yatima, wazee na wenye ulemavu.
“Ninawatakia heri viongozi wa Serikali, akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Mheshimiwa Hajjat Fatuma Mwassa, pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Mheshimiwa Erasto Sima, pamoja na viongozi wa Chama ngazi zote. Nawapongeza na kuwaombea afya njema, amani na mafanikio katika utekelezaji wa majukumu yao ya kuwatumikia wananchi wa Mkoa wa Kagera,” amesema Mbunge Johnston Mutasingwa.
Kadhalika, Mhandisi Mutasingwa amewashukuru wananchi wa Jimbo la Bukoba Mjini kwa kumuamini na kumpigia kura nyingi katika Uchaguzi Mkuu, akiahidi kuendelea kuwatumikia kwa uaminifu, uwazi na kujali maslahi ya jamii.
Sikukuu ya Krismasi huadhimishwa Desemba 25 kila mwaka na mamilioni ya waumini wa dini ya Kikristo duniani kote, ikiwa ni kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo, tukio linalohimiza amani, upendo na matumaini mapya kwa wanadamu.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment