
Timu ya taifa ya soka ya wanaume Tanzania ( Taifa Stars) imeanza kampeni yake ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2025) kwa kupokea kipigo cha mabao 2-1 dhidi ya vigogo Nigeria, katika mchezo wa Kundi C uliochezwa leo Desemba 23, 2025, nchini Morocco.
Nigeria walitangulia kupata bao dakika ya 36 ya kipindi cha kwanza kupitia kwa mshambuliaji wao Alex Iwobi. Taifa Stars walifanikiwa kusawazisha dakika ya 50 kupitia kwa Charles William M’Mombwa, na kurejesha matumaini kwa mashabiki wa Tanzania.
Hata hivyo, dakika mbili baadaye, yaani dakika ya 52, Nigeria walipata bao la pili kupitia kwa Ademola Lookman, na hatimaye kuondoka na pointi tatu muhimu katika Kundi C.
Licha ya kupoteza mchezo huo, Taifa Stars chini ya kocha Miguel Gamondi walionesha upinzani mkubwa, wakicheza kwa nidhamu na kujiamini. Kikosi hicho kilikuwa na wachezaji wanaocheza nje ya nchi pamoja na nyota wa ndani kutoka klabu za Simba SC, Young Africans (Yanga) na Azam FC.
Huu ni ushiriki wa nne wa Tanzania katika fainali za AFCON, Taifa Stars wamepangwa katika Kundi C, linalotajwa kuwa miongoni mwa makundi magumu zaidi, likijumuisha Nigeria, Tunisia na Uganda.
Nigeria na Tanzania zimekutana katika fainali za AFCON kwa mara ya pili. Mara ya kwanza ilikuwa mwaka 1980, ambapo Nigeria waliifunga Tanzania 3-1 katika mechi ya ufunguzi iliyochezwa Lagos, kabla ya kutwaa ubingwa wao wa kwanza wa Afrika.
Kwa ujumla, timu hizo zimekutana mara nane katika mashindano yote. Nigeria bado hawajawahi kufungwa na Tanzania, wakishinda mechi tano na kutoka sare tatu.
Mara ya mwisho timu hizo kukutana ilikuwa katika mechi za kufuzu AFCON 2017, ambapo walitoka sare ya 0-0 jijini Dar es Salaam, kabla ya Nigeria kushinda 1-0 katika mchezo wa marudiano uliochezwa mjini Uyo.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment