" UMOJA WA WAZAZI MPANDA WAFANYA KIKAO CHA KAWAIDA CHA KAMATI YA UTEKELEZAJI, WATATHMINI MAFANIKIO YA 2025

UMOJA WA WAZAZI MPANDA WAFANYA KIKAO CHA KAWAIDA CHA KAMATI YA UTEKELEZAJI, WATATHMINI MAFANIKIO YA 2025

Umoja wa Wazazi Wilaya ya Mpanda umefanya kikao cha kawaida cha kikanuni cha Kamati ya Utekelezaji wa Wazazi Wilaya ya Mpanda leo tarehe 22 Desemba 2025 kwa lengo la kujadili utekelezaji wa majukumu ya jumuiya hiyo kwa kipindi cha mwaka 2025.

Kikao hicho kimefunguliwa majira ya saa 4:00 asubuhi na Mwenyekiti wa Umoja wa Wazazi Wilaya ya Mpanda, ndugu Pius Buzumalle, ambaye anawahimiza wajumbe kujadili kwa uwazi, kutoa maoni yenye kujenga na kushiriki kikamilifu ili kuimarisha umoja na mshikamano ndani ya jumuiya.

Katibu wa Umoja wa Wazazi Wilaya ya Mpanda, ndugu Jimotoli Jilala Maduka, amewakaribisha wajumbe wote walioudhuria kikao hicho na kueleza kuwa ajenda kuu ni kujadili utekelezaji wa shughuli za jumuiya kwa kipindi cha Januari hadi Desemba 2025 pamoja na kufanya tathmini ya mafanikio yaliyopatikana.

Katika kikao hicho, Kamati ya Utekelezaji imejadili mafanikio mbalimbali yaliyofikiwa ikiwemo ujenzi wa shule ya sekondari ya ufundi Milala iliyopo Kata ya Misunkumilo, Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda, ambapo jumuiya imepongeza kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo katika kusukuma mbele elimu ya ufundi.

Vilevile, kikao kimejadili uhai wa jumuiya kwa kuzingatia kuongezeka kwa wanachama wapya na urejeshaji wa wanachama waliokuwa hawashiriki kikamilifu, hali inayochangia kuimarika kwa shughuli za Umoja wa Wazazi wilayani humo.

Ajenda nyingine ni taarifa ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025, ambapo wajumbe wameeleza kuridhishwa na ushindi mkubwa wa Chama Cha Mapinduzi chini ya uongozi wa Mwenyekiti wa CCM Taifa, Dkt. Samia Suluhu Hassan, na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Pia, kikao kimejadili ushindi wa Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Nsimbo, ambapo Umoja wa Wazazi unaelezwa kupata nafasi ya kushirikiana na viongozi hao katika kutekeleza majukumu ya jumuiya.

Mwisho wa kikao, Mwenyekiti ndugu Pius Buzumalle amewapongeza wajumbe kwa michango yao na kumpongeza Katibu kwa maandalizi ya kikao, huku akiwataka viongozi na wanachama kuendelea kushikamana, kuwajibika na kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi zaidi.

 

Post a Comment

Previous Post Next Post