Baada ya Watanzania kukataa kwa nguvu zote kurudi kwenye machungu ya migogoro ya kisiasa, wametoa wito wa kitaifa wa kudumisha amani, wakisisitiza kuwa utulivu wa nchi ni msingi wa ushirikiano wa kimataifa na kuvutia wawekezaji, hatua muhimu kuelekea Dira 2050.
Wananchi wameeleza bayana kwamba machungu ya Oktoba 29 yalitosha na hawatakubali tena kurudi kwenye machungu na majuto, wakisema wameona "waliochochea fujo wanakula bata" huku wakiendelea kutia utambi kwa wananchi. Wameamua kuamka na kusema "basi, inatosha!" na kuchagua ustahimilivu na mazungumzo.
Kinyume na sauti za uchochezi zinazovuruga amani, Watanzania wanakumbushwa kwamba vurugu na mizozo huua ushirikiano na kukimbiza wawekezaji, na hivyo kudhoofisha ujenzi wa uchumi wa taifa.
Bernard Zephan, Mkazi wa Dodoma, anaeleza jukumu la amani kwenye jukwaa la kimataifa:
“Amani huleta uhusiano mzuri kimataifa na ushirikiano wa kikanda, Tanzania yenye amani hujenga taswira nzuri duniani na kufungua milango ya biashara na diplomasia, hivyo kuchangia ustawi wa wananchi na maendeleo ya kitaifa,” anasema Bw. Zephan.
Hakuna mwekezaji wa kimataifa anayeweza kuhatarisha mtaji wake katika nchi yenye migogoro, vurugu, au uasi. Ghasia za baada ya uchaguzi huonyesha ukosefu wa utabiri wa kiuchumi (economic predictability), na kusababisha wawekezaji kuhamisha miradi yao kwenda nchi zenye amani na utulivu.
Kuharibu Diplomasia: Migogoro ya ndani inadhoofisha uwezo wa Tanzania kujenga uhusiano mzuri wa diplomasia na kuzuia mikataba muhimu ya kimataifa, hivyo kupunguza fursa za biashara na misaada ya maendeleo.
Wananchi wamejifunza kwamba madhara ya migogoro huangukia kwao moja kwa moja—uharibifu wa mali, uhamaji, na matumizi ya rasilimali bila mpangilio kama anavyosema Amina Mbisa, Mkazi wa Songwe.
“Oktoba 29, 2025 tulijikuta kwenye changamoto chungu nzima, madhara yalikuwa mengi tulioathirika ni sisi wananchi wenyewe, kwa kipindi kichache tumejifunza umuhimu wa amani na kwa nini tunapaswa kuilinda,” anasema Bi. Amina.
Kwa msingi huu, Watanzania wamekubali kuchagua ustahimilivu, wakisisitiza kwamba watatumia mifumo ya ndani kuondoa hitilafu na kukubaliana kutokukubaliana—msimamo unaoendana na ajenda ya 4R ya Rais Samia ya maridhiano na ustahimilivu.
"Kwenye jamii yenye amani kuna weledi na utaratibu katika usimamizi wa rasilimali jambo ambalo huchochea maendeleo endelevu na kizazi cha sasa na kijacho kunufaika.” anasema Jackson John, Mkazi wa Dodoma.
Msimamo wa Watanzania wa kukataa sauti za uchochezi na kudumisha amani ni uamuzi wa kiuchumi. Kwa kuendelea kuwa wastahimilivu na kuchagua mazungumzo, nchi inajilinda kiuchumi, inajenga taswira bora kimataifa, na inahakikisha rasilimali zetu zinatumika kwa weledi na utaratibu ili kufanikisha DIRA 2050.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment