
Lucy Antony Michael (35), Mkazi wa Yombo Dovya, Mtaa wa Makangarawe, Wilayani Temeke, Dar es Salaam amevamiwa na watu wasiojulikana akiwa anatoka nyumbani kwake, ambapo watu hao walimpiga na kumshambulia maeneo mbalimbali ya mwili wake
Lucy ambaye ni miongoni mwa watu waliojitambulisha kuwa ni Waumini wa Kanisa Katoliki walioenda kwenye Ubalozi wa Vatican, uliopo hapa nchini kwaajili ya kupeleka barua ya malalamiko juu ya mwenendo wa baadhi ya viongozi wa Kanisa hilo hivi karibuni, amesema kabla ya kuvamiwa na kushambuliwa kwake kwa siku kadhaa amekuwa kwenye misukosuko ya kupokea simu na kutumiwa sms za kejeli, matusi na wengine kumtishia maisha
Akizungumza na Waandishi wa Habari akiwa nyumbani kwake leo, Jumapili Januari 11.2026, Lucy amehusianisha kushambuliwa kwake na maoni aliyotoa mbele ya Wanahabari kuhusiana na mwenendo wa baadhi ya viongozi wa Kanisa Katoliki, jambo ambalo ameeleza kuwa amelifanya kwa nia njema ya kujenga iliyolenga kuwarejesha viongozi hao kwenye mstari, maoni ambayo yamepokelewa kwa hisia hasi kwa baadhi watu kwenye jamii
Aidha, bada ya kushambuliwa Lucy amefikisha malalamiko yake kwenye Kituo cha Polisi Makangarawe na kupewa RB No. MAR/RB/49/2026
Shuhuda wa tukio hilo Sabina Michael, Mjumbe wa Serikali ya Mtaa Ashura Salum na Daud Leonard ambaye ni mmoja wa waumini wanaosali pamoja na Lucy, kwa nyakati tofauti wameeleza kusikitishwa na tukio hilo sambamba na kuziomba mamlaka husika kuchukua hatua stahiki kwa wote waliohusika, huku pia wakiomba kuimarishiwa zaidi usalama mtaani kwao kwani matukio ya aina hiyo yanaweza kusababisha wasiwasi kwa jamii.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment