Na Lydia Lugakila Kagera Leo, Januari 27, ni siku ya kipekee na ya kihistoria kwa Watanzania, ikiwa ni siku ya kuzaliwa ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan. Katika kuadhimisha siku hii muhimu, Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Kagera, chini ya uongozi mahiri wa Mwenyekiti wao, Faris Buruhan, umeandaa tukio la uzalendo na lenye kugusa maisha ya wananchi moja kwa moja. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Faris Buruhan ametaja siku hii kuwa ni “Birthday ya kibabe”, akiwakaribisha vijana na wananchi kushiriki tukio la pamoja litakalofanyika katika Shule ya Sekondari Omumwani, Manispaa ya Bukoba, kuanzia asubuhi. Katika maadhimisho hayo, UVCCM Kagera wanatarajia kupanda miti 2,000, kukata keki, pamoja na kumuimbia Rais Samia nyimbo za pongezi na kumtakia heri, baraka na afya njema anapoadhimisha siku yake ya kuzaliwa. Akisisitiza uzalendo wa vitendo, Faris Buruhan ameeleza kuwa “Uzalendo wa kweli ni kutunza mazingira”, akiwahimiza vijana na wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki zoezi hilo la upandaji miti kama ishara ya kumuunga mkono Rais Samia katika jitihada zake za kulinda mazingira na kuijenga Tanzania endelevu. Tukio hili linaonesha mshikamano, upendo na heshima kubwa ya vijana wa CCM Kagera kwa Rais Samia Suluhu Hassan, kiongozi mwenye maono, mama wa taifa, na mfano wa uongozi bora barani Afrika.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment