" CLATOUS CHAMA AREJEA SIMBA SC

CLATOUS CHAMA AREJEA SIMBA SC






Kiungo mahiri, Clatous Chama, amejiunga na Simba Sports Club, baada ya klabu hiyo kukamilisha taratibu zote za usajili wake.

Chama, ambaye alikuwa akiitumikia Singida Black Stars, amecheza mechi yake ya mwisho leo akiwa na jezi ya klabu hiyo katika Uwanja wa KMC Complex, kabla ya kuanza safari mpya ndani ya kikosi cha Wekundu wa Msimbazi.

Usajili wa Chama unaifanya Simba kumrudisha tena kiungo ambaye aliwahi kuwa mhimili muhimu wa mafanikio ya klabu hiyo katika misimu iliyopita, akitambulika kwa uwezo mkubwa wa kusoma mchezo, kutoa pasi za mwisho na kuiongoza safu ya kiungo kwa utulivu na ubunifu.

Uzoefu wake katika mashindano ya ndani na ya kimataifa unatajwa kuwa sababu kubwa ya Simba kuamua kumrejesha kikosini.

 

Post a Comment

Previous Post Next Post