" EAST AFRICAN SPIRITS YAZIDI KUNG’ARA KATIKA SEKTA YA VIWANDA NCHINI

EAST AFRICAN SPIRITS YAZIDI KUNG’ARA KATIKA SEKTA YA VIWANDA NCHINI

Mafanikio ya Kampuni ya East African Spirits (T) Ltd yanaendelea kuonesha dhamira ya uwekezaji wenye tija, unaochochea ajira, kuongeza mapato ya Serikali na kukuza uchumi wa wananchi kwa vitendo.

MAWASILIANO YA KAMPUNI – EAST AFRICAN SPIRITS (T) LTD
📞 +255 767 650 806
📞 +255 652 096 254
📧 info@eastafricanspirits.com
🌐 www.eastafricanspirits.com

East African Spirits – ubora wa kitanzania, hadhi ya kimataifa

Mkurugenzi wa Kampuni ya East African Spirits (T) Limited (EASTL), Bw. Gaspar Kileo, akimuongoza Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Mipango na Uwekezaji, Mhe. Dkt. Pius Stephen Chaya (kulia), kutembelea maeneo mbalimbali ya uzalishaji katika kiwanda hicho mkoani Shinyanga.

Na Kadama Malunde 

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Mipango na Uwekezaji, Mhe. Dkt. Pius Stephen Chaya, amepongeza uwekezaji mkubwa wa kizalendo uliofanywa na mwekezaji mzawa kupitia Kampuni ya East African Spirits (T) Limited (EASTL) mkoani Shinyanga, akisema uwekezaji huo ni mfano halisi wa uwekezaji wenye tija unaotekeleza kwa vitendo dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita ya kukuza uchumi wa taifa, kuunda ajira kwa Watanzania na kuongeza mapato ya Serikali.

Dkt. Chaya ametoa pongezi hizo leo Januari 9, 2026, wakati wa ziara yake ya kikazi katika Kiwanda cha Uzalishaji wa Vinywaji Vikali kinachomilikiwa na EASTL kilichopo mkoani Shinyanga, ambapo alijionea shughuli za uzalishaji na kueleza kuridhishwa na mchango wa uwekezaji huo katika kuchochea ajira, kukuza pato la taifa na kuimarisha ustawi wa kiuchumi wa wananchi.

Akizungumza mara baada ya kutembelea maeneo mbalimbali ya uzalishaji, mitambo na maabara ya kisasa ya kiwanda hicho, Dkt. Chaya amesema ameridhishwa na uwekezaji uliofanywa na mwekezaji mzawa, Bw. Gaspar Kileo, aliyefanikiwa kuwekeza zaidi ya Shilingi Bilioni 30 mkoani Shinyanga, badala ya kupeleka mitaji yake nje ya nchi.
Mkurugenzi wa Kampuni ya East African Spirits (T) Limited (EASTL), Bw. Gaspar Kileo, akimkaribisha Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Mipango na Uwekezaji, Mhe. Dkt. Pius Stephen Chaya, kabla ya kutembelea maeneo mbalimbali ya uzalishaji katika kiwanda hicho mkoani Shinyanga.

“Leo nimekuja hapa kwenye kiwanda cha mwekezaji mzawa Gaspar Kileo ambaye amewekeza zaidi ya shilingi bilioni 30 hapa Shinyanga. Nichukue fursa hii kumpongeza kwa uzalendo wake. Ameamua kuwekeza hapa nyumbani, ameweka mitambo ya kisasa kabisa na maabara ya viwango vya juu,” amesema Dkt. Chaya.

Naibu Waziri amesisitiza kuwa uwekezaji huo ni mfano hai wa dira ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, inayosisitiza uwekezaji wenye tija unaozalisha ajira, kukuza pato la taifa na kuongeza kipato cha wananchi mmoja mmoja.

Kwa mujibu wa taarifa alizopewa, kiwanda hicho kinachangia zaidi ya Shilingi Bilioni 20 kwa mwaka kama kodi kwa Serikali, hatua inayochangia moja kwa moja katika mapato ya taifa na uwezo wa Serikali kutoa huduma za jamii.

Aidha, kiwanda kimezalisha ajira zaidi ya 200 za moja kwa moja, pamoja na ajira zisizo za moja kwa moja kupitia mnyororo wa thamani.

Dkt. Chaya ameeleza kuwa uzalishaji wa bia, wine na spirit unahitaji malighafi kama shayiri (barley), inayolimwa na wakulima , jambo linalokuza sekta ya kilimo na kuwaongezea wakulima kipato na kwamba kwa sasa wakulima wanaonufaika na uwekezaji huo wanatoka maeneo mbalimbali, hususan Kanda ya Kaskazini.

“Huu ni uwekezaji unaogusa maisha ya wananchi wengi. Unachochea kilimo, unazalisha ajira kwa waliosoma na wasiosoma, na unaongeza mapato ya taifa. Hii ndiyo adhima ya Serikali,” ameongeza Dkt. Chaya.
Katika ziara hiyo, Naibu Waziri pia amebainisha changamoto ya upungufu wa chupa za kufungashia vinywaji, na kuitaja kama fursa mpya ya uwekezaji.

Ametoa wito kwa wawekezaji wengine kuwekeza katika viwanda vya kuzalisha chupa, akieleza kuwa kwa sasa mwekezaji wa chupa nchini yupo Dar es Salaam pekee.

Amekumbusha kuwa Serikali ipo katika mpango wa kuanzisha Kongani za Viwanda katika kila wilaya, kwa maelekezo ya Rais Samia, na hivyo kuwepo kwa fursa kubwa kwa wawekezaji wanaotaka kuingia kwenye sekta ya vifungashio.

“Tunapofuatilia uwekezaji, tunaangalia je uwekezaji una tija? Je unazalisha ajira? Na je unahusisha mnyororo wa thamani na kukuza pato la taifa? Uwekezaji huu unajibu maswali yote hayo,” amesisitiza.

Awali, akisoma risala ya uongozi wa East African Spirits (T) Ltd kwa mgeni rasmi, Mkurugenzi Msaidizi wa Masoko na Uongozi wa kampuni hiyo, Godbless Gaspar Kileo, amesema ziara ya Naibu Waziri ni uthibitisho wa dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita katika kuwawezesha na kuwaunga mkono wawekezaji wazalendo.
Mkurugenzi Msaidizi wa Masoko na Uongozi wa Kampuni ya East African Spirits (T) Limited (EASTL), Bw. Godbless Gaspar Kileo.

Ameeleza kuwa safari ya ujenzi wa kiwanda hicho ilianza Oktoba 2019, kwa lengo la kuongeza thamani ya mazao ya kilimo mkoani Shinyanga. Baada ya ujenzi na usimikaji wa mitambo, kiwanda kilizinduliwa rasmi Machi 2023, na tangu hapo kimekuwa kikizalisha bidhaa kwa kuzingatia viwango vya ubora na ushindani wa soko.

Amesema hadi sasa uwekezaji katika mradi umefikia Shilingi Bilioni 34, ukihusisha ushirikiano wa karibu na wadau wa maendeleo, hususan Benki ya CRDB, iliyosaidia kukamilisha miundombinu na ununuzi wa mitambo ya kisasa.

Kampuni hiyo imesema manufaa ya uwekezaji wake yameonekana wazi kwa Taifa na jamii, ikiwemo ajira zaidi ya 200 za moja kwa moja, ongezeko la mapato ya Serikali, pamoja na kukuza kipato cha wakulima wanaolima shayiri kutoka Hanang (Manyara), West Kilimanjaro na Siha.

Aidha, kiwanda kimekuwa mshirika wa karibu wa jamii inayokizunguka kwa kutoa fursa za kiuchumi kwa Mama Lishe, wabeba mizigo na watoa huduma wadogo wadogo, hatua inayochochea uchumi wa ndani wa Manispaa ya Shinyanga.
Amesema uongozi wa East African Spirits (T) Ltd unaiomba Serikali kuendelea kuwalinda na kuwasaidia wawekezaji wazalendo, hususan katika changamoto za ushindani wa soko na miundombinu, ili kuongeza uzalishaji, kupanua masoko ya ndani na nje ya nchi, na kuingiza zaidi fedha za kigeni nchini.

Katika ziara hiyo, Dkt. Chaya pia ametembelea Kiwanda cha Uzalishaji wa Vinywaji Vikali cha East African Spirits (T) Limited (EASTL) pamoja na Kiwanda cha Nyama kilichopo Old Shinyanga, ambapo alisema eneo hilo lipo wazi kwa uwekezaji na kuwataka wawekezaji kujitokeza kuwekeza.

Uwekezaji wa kizalendo unaendelea kujidhihirisha kuwa mhimili muhimu wa maendeleo ya Taifa, hususan unapoungwa mkono na sera madhubuti na mazingira rafiki ya Serikali, hali inayojenga uchumi jumuishi, shindani na wenye tija unaolenga kuongeza ajira, kukuza pato la taifa na kuimarisha ustawi wa Watanzania kwa maendeleo endelevu ya Tanzania.

Mkurugenzi Msaidizi wa Masoko na Uongozi wa Kampuni ya East African Spirits (T) Limited (EASTL), Bw. Godbless Gaspar Kileo, akisoma risala ya uongozi wa kampuni hiyo kwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Mipango na Uwekezaji, Mhe. Dkt. Pius Stephen Chaya, wakati wa ziara katika kiwanda hicho mkoani Shinyanga.
Mkurugenzi Msaidizi wa Masoko na Uongozi wa Kampuni ya East African Spirits (T) Limited (EASTL), Bw. Godbless Gaspar Kileo, akisoma risala ya uongozi wa kampuni hiyo kwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Mipango na Uwekezaji, Mhe. Dkt. Pius Stephen Chaya, wakati wa ziara katika kiwanda hicho mkoani Shinyanga.
Mkurugenzi wa Kampuni ya East African Spirits (T) Limited (EASTL), Bw. Gaspar Kileo, akimueleza Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Mipango na Uwekezaji, Mhe. Dkt. Pius Stephen Chaya (kulia), kuhusu mchakato wa uzalishaji wa vinywaji katika kiwanda hicho.
Mkurugenzi wa Kampuni ya East African Spirits (T) Limited (EASTL), Bw. Gaspar Kileo, akimueleza Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Mipango na Uwekezaji, Mhe. Dkt. Pius Stephen Chaya (kulia), kuhusu mchakato wa uzalishaji wa vinywaji katika kiwanda hicho.
Mkurugenzi wa Kampuni ya East African Spirits (T) Limited (EASTL), Bw. Gaspar Kileo, akimuongoza Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Mipango na Uwekezaji, Mhe. Dkt. Pius Stephen Chaya, kutembelea maeneo mbalimbali ya uzalishaji katika kiwanda hicho mkoani Shinyanga.
Mkurugenzi wa Kampuni ya East African Spirits (T) Limited (EASTL), Bw. Gaspar Kileo, akimuongoza Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Mipango na Uwekezaji, Mhe. Dkt. Pius Stephen Chaya, kutembelea maeneo mbalimbali ya uzalishaji katika kiwanda hicho mkoani Shinyanga.
Mkurugenzi wa Kampuni ya East African Spirits (T) Limited (EASTL), Bw. Gaspar Kileo, akimuongoza Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Mipango na Uwekezaji, Mhe. Dkt. Pius Stephen Chaya, kutembelea maeneo mbalimbali ya uzalishaji katika kiwanda hicho mkoani Shinyanga.
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Mipango na Uwekezaji, Mhe. Dkt. Pius Stephen Chaya, alipotembelea kiwanda cha Kampuni ya East African Spirits (T) Limited (EASTL) mkoani Shinyanga.


Kampuni ya East African Spirits (T) Limited (EASTL) inajihusisha na uzalishaji wa vinywaji mbalimbali vikiwemo vinywaji vikali na bia, ambapo miongoni mwa bidhaa zake ni pombe kali kama Hanson’s Choice Brandy na Diamond Rock Gin, pamoja na bia za aina tofauti zikiwemo Goldberg Malt LagerHanson’s Lite Lager na Basembi Extra Lager, ambazo zote huzalishwa kwa kuzingatia viwango vya ubora na ushindani wa soko, zikiwa na lengo la kukidhi mahitaji ya watumiaji wa ndani na kukuza tasnia ya vinywaji nchini kupitia malighafi za kilimo cha wazawa.

 

Post a Comment

Previous Post Next Post