Na Mapuli Kitina Misalaba
Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga imeanza rasmi kutoa huduma za afya za kibingwa ikiwemo huduma za daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake na uzazi kila siku pamoja na kliniki ya daktari bingwa wa mifupa (Orthopedic) kila Jumamosi, hatua inayolenga kuwasogezea wananchi huduma muhimu karibu zaidi na kuwasaidia kupunguza gharama walizokuwa wakizitumia kusafiri hadi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga iliyopo Mwamwaza.
Akizungumza kuhusu huduma hizo, Mganga Mfawidhi (MOI) wa Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga, Dkt. Pierina Mwaluko, amesema ujio wa madaktari bingwa katika hospitali hiyo ni mkombozi mkubwa kwa wakazi wa Manispaa ya Shinyanga na mkoa kwa ujumla.
“Kwa muda mrefu wananchi walilazimika kusafiri umbali mrefu na kutumia gharama kubwa kufuata huduma za kibingwa. Sasa huduma hizo zinapatikana moja kwa moja hapa Manispaa ya Shinyanga,” amesema.
Dkt. Mwaluko ameongeza kuwa huduma nyingi za kibingwa zilizokuwa zinapatikana Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwawaza sasa zinapatikana Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga, jambo linalosaidia kupunguza msongamano katika hospitali ya rufaa na kuongeza ufanisi wa utoaji wa huduma za afya kwa wananchi.
Amebainisha kuwa hospitali imejipanga vyema kuhudumia wagonjwa wa nje na wa ndani, ikiwa na jengo la OPD lenye miundombinu ya kisasa na wodi ya wanawake iliyoboreshwa kwa ajili ya huduma za ndani na kwamba hospitali ina vifaa vya kisasa vya uchunguzi, ikiwemo maabara iliyoimarishwa na huduma za mionzi kama ultrasound, zinazosaidia kubaini magonjwa haraka na kwa usahihi.
Kwa upande wa huduma za upasuaji, Dkt. Mwaluko amesema hospitali ina jengo la upasuaji (theatre) lililoandaliwa kwa viwango vinavyotakiwa, likiwa na chumba cha upasuaji chenye vifaa muhimu kwa wagonjwa wanaohitaji huduma hizo.
Kwa upande wake, Dkt. Elipidius Theodory, Daktari Bingwa wa Uzazi na Magonjwa ya Wanawake, amesema hospitali inatoa huduma za uchunguzi na matibabu ya changamoto mbalimbali za afya ya uzazi kwa akina mama, ikiwemo matatizo ya mfumo wa uzazi, huduma za uchunguzi wa saratani, uzazi wa mpango pamoja na ufuatiliaji wa wajawazito, wakiwemo wenye mimba hatarishi.
Uongozi wa Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga umehitimisha kwa kuwakaribisha wananchi wote wa Mkoa wa Shinyanga na mikoa ya jirani kufika hospitalini hapo kupata huduma za kibingwa, ukisisitiza kuwa sasa huduma hizo zinapatikana karibu, kwa ubora na kwa gharama nafuu.
Mganga Mfawidha wa Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga Dkt. Pierina Mwaluko, akizungumza na Misalaba Media.

Daktari Bingwa wa Uzazi na Magonjwa ya Wanawake Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga Dkt. Elipidius Theodory, akizungumza.
Baadhi ya majengo ya Hospitali ya Manispaa ya Shinyanga yakiwa na miundombinu ya kisasa kwa ajili ya utoaji wa huduma za afya kwa wananchi.🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
















Post a Comment