" IJUE KAGERA: HISTORIA, MAKABILA NA VITEGA UCHUMI VINAVYOUBEBA MKOA:

IJUE KAGERA: HISTORIA, MAKABILA NA VITEGA UCHUMI VINAVYOUBEBA MKOA:


Na: Mbeki Mbeki.

Kagera.

Mkoa wa kagera,ulioko kaskazini magharibi mwa Tanzania,ni moja ya maeneo yenye historia ya kipekee.

Kabla ya uhuru ,eneo hili lilijukana kama West lake( ziwa magharibi) kutokana na nafasi 

Yake magharibi mwa ziwa Victoria.  

Jina hilo lilibadilishwa baada ya vita ya kagera ,(1978 hadi 1979) kuenzi uzalendo na ushindi wa Tanzania dhidi ya uvamizi wa uganda ,likabeba jina la mto kagera ,alama ya mpaka uliotetewa kwa nguvu ya taifa.

Makabila ya kagera: Mkoa huu unajumuisha makabila yenye asili ya kihistoria ya wahaya,wanyambo,wahangaza,wasubi,waha,na wazinza.

* Wahaya wanapatikana zaidi, Bukoba ,misenyi na Muleba.

* Wanyambo:( Nyambo) zaidi karagwe na kyerwa.

* Wahangaza,Ngara.

* Wasubi,Biharamulo.

* Wazinza & wasukuma kwasehemu  Biharamulo na chato ,( Zamani ndani ya kagera kabla ya kuhamia Geita).

Vitega uchumi vikuu vya mkoa.

1. Kilimo uti wamgongo wa mikoa.

Kagera ni maarufu kwa uzalishaji wa:

* Kahawa ( Robusta) zao kuu la biashara ,hasa Bukoba muleba,karagwe,misenyi, na kyerwa.

* chai,mashamba makubwa maarufu & Mbonde (Bukoba).

* Tumbaku zaidi Ngara na Biharamulo.

* Vanilla,maharage,mahindi,viazi mviringo.

2: Uvuvi ziwa Victoria.

Uvuvi wa sangara ( Nile perch), Sato na dagaa unachangia ajira na mapato kwa wananchi wa ukanda wa ziwa.

3. Misitu na Asali.

Wilaya za Biharamulo na Muleba zina rasilimali za misitu zikisaidia:

* Uzalishaji wa mbao.

* Asali na nta ,kupitia vikundi vya ufugaji nyuki.

4: Madini: 

* Biharamulo inahifadhi za dhahabu na uchimbaji mdogo wa madini.

* Eneo la mkoa liko ndani ya ukanda wa dhahabu wa ziwa Victoria ( Lake Victoria Gold belt).

5: Utalii.

* Ziwa ni pamoja na: fukwe zake (Bukoba).

* Maporomoko ya Rusumo ( Ngara) historia ya ukombozi wa Rwanda 1994.

* Hifadhi ya Burigi_ Chato ,( zamani sehemu ya kagera kabla ya mabadiliko ya mipaka ya kiutawala).

* Utamaduni wa wahaya ( mila,chakula,ngoma na urithi wa kifalme).

* Biashara ya mipakani.

* Hifadhi ya Rumanyika orugundu.

* Mtagata( water sprig 40 centigrade).

Kagera inapakana.

* Uganda.

* Rwanda.

* Burundi.

Hali hii inaiwezesha kuwa  kitovu cha biashara za kuvuka mipaka ,  hasa Ngara na Kyerwa.

Miundo mbinu ya kiuchumi.

Mkoa umewekeza pia katika.

* Viwanda vya kuchakata  kahawa.

* Viwanda vidogovidogo vya maziwa.

* Vyama vya ushirika ( AMCOS) vinavyosaidia wakulima wa kahawa.

* Kiwanda cha sukari( kagera sugar).

Kagera ni mkoa unaosimama kwenye historia ya uzalendo ,ukijivunia utoamuzi wa makabila mbalimbali na uchumi unaochangizwa na kilimo,uvuvi,madini na biashara ya mipakani.

Aidha,Mkuu wa mkoa wa kagera wasasa 2025/2026 ni mh. Hajat Fatma Abubakary Mwassa ,yeye ndiye anayeongoza utendaji kazi wa serikali mkoani humo,kusimamia maendeleo ,utekelezaji wa sera za serkali na usimamizi wa maeneo ya mkoa.

Post a Comment

Previous Post Next Post