
Pichani ni Ol-aiguenani Meshack Meliyo Ndaskoi ambaye amechaguliwa kuwa Mkuu wa jamii ya Wamaasai waishio Dar es Salaam na Pwani.


……..
Na Happy Lazaro, Dar es Salaam.
Tangu enzi za kale, jamii ya Wamaasai imekuwa na utaratibu wa kuwa na viongozi wa jadi Il-aiguanak ambao huchaguliwa na watu kuwaongoza na kwa mujibu wa taratibu zao kila mtu popote alipo anakuwa chini ya kiongozi.
Kutokana na hali hii Wamaasai waishio Dar es Salaam na Pwani waliwachagua viongozi wao wa kuwaongoza ambao walisimikwa na Il-aiguenak wa Baraza la Marya wakiongozwa na Ol-aiguenani Mkuu wa jamii ya Wamaasai Tanzania Isack Meijo Ole Kisongo.
Hafla ya kuwasimika viongozi hao ilienda sambamba na uzinduzi wa Mkoa wa kiutawala wa jadi ambayo inajulikana kwa Kimaasai E–mbalbal e Dar es Salaam o Pwani.
Aidha Il-aiguanak wa E-mbalmbal katika kikao kilichofanyika hivi karibuni kwa kauli moja walimchagua Ol-aiguenani Meshack Meliyo Ndaskoi kuwa Ol-ainguenani Mkuu wa jamii ya Wamaasai waishio Dar es Salaam na Pwani.
Wakati Ol-aiguenani Ndaskoi akizungumza mara baada ya kukabidhiwa mamlaka hayo, aliahidi kuekeleza majukumu yake kwa kuendeleza mshikamano miongoni mwa jamii ya Wamaasai na kusimamia na kuimarisha utamaduni, mila na desturi nzuri ya jamii ya Wamaasai ambayo ni sehemu ya utamaduni wa Mtanzania kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zilizopo kwa ajili ya manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.
Aidha ameweka wazi masuala ya kipaumbele katika kipindi chake cha uongozi wake kama ifuatavyo: –
“Nitajitahidi kuunganisha jamii ya Wamaasai waishio Dar es Salaam na Pwani ili waweze kudumisha upendo, amani ushirikiano na mshikamano miongoni mwao.”amesema
Aidha amesema kuwa atahakikisha kwamba jamii ya Wamaasai inaenzi kwa kuendeleza mila ya rika ambayo ni muhimu sana katika kudumisha kuheshimiana mshikamano, upendo, maadili mema, ujasiri.
Aidha amesema atahakikisha vijana wanapata elimu ili kuwajenga kimaadili kutokana na kumekuwepo na kuporomoka kwa maadili kwa kiwango kikubwa katika jamii hususan mongoni mwa vijana kinachochangiwa kwa kiwando kikubwa na utandawazi, jambo linalohitaji kuchukua hatua za makusudi na haraka ili kuwanusuru vijana na kuhakikisha hawaondoki kwenye maadili mema.
Ameongeza kuwa , atadumisha njia za jamii ya jadi ya Wamaasai za utatuzi wa migogoro na upatanisho kwa kutumia sheria, taratibu na kanuni za jadi ambazo hudumisha upendo, amani na kuondoa mifarakano.
“Nitatahakikisha kwamba jamii ya Wamaasai inaenzi utamaduni na mila kwa kulinda, kuhifadhi, kuendeleza na kutangaza utamaduni, kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho. “amesema .
Amesisitiza na kuahidi kwamba katika kutekeleza majukumu yake atashirikiana na Serikali katika ngazi zote, wadau wengine pamoja na jamii nzima kwa kuwa mafanikio ya kudumisha utamaduni na mila ili kuleta mandeleo endelevu ya jamii yanategemea sana utashi, ushirikiano na mshikamano wa wadau wote.
Aidha amezungumzia changamoto kubwa inayokabili utamaduni na mila hihi sasa alisema, katika kipindi hiki cha utandawazi jitihada kubwa inahitajika kutoka kwa wadau wote kwa sababu unaweza kuwa na athari mbaya kwa tamaduni zetu kwa kuwa inalenga kusawazisha na kuanzisha ushawishi wa chapa za kigeni ambapo unaweza kuchangia kupoteza utambulisho wa kitamaduni.
“Natoa wito kwa viongozi katika ngazi zote pamoja na wazazi kujitahidi kuwa mfano mzuri wa kuingwa katika jamii ili kujenga jamii yenye kufuata maadili mema kwani wao ndio kioo cha jamii mahali popote pale wanapokuwa. “amesema”.
Post a Comment