Kampuni ya CHICO inayojenga kiwanja cha ndege cha
Shinyanga imetekeleza ombi la Diwani wa Kata ya Kolandoto Mhe. Moses Mshagatila,
kwa kuboresha barabara ya Kolandoto Hospital, ambayo ilikuwa imeharibika.
Hatua hiyo imetokana na ziara ya Diwani Mshagatila
katika kampuni hiyo, ambapo aliwasilisha ombi maalumu kutoka kwa Mbunge wa
Jimbo la Shinyanga Mjini, Mheshimiwa Paschal Patrobas Katambi, ambaye pia ni
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.
Baada ya ziara hiyo na ombi rasmi la diwani, kampuni
ya CHICO mara moja ilichukua hatua za ukarabati na barabara ya Kolandoto tayari
imeboreshwa kikamilifu, ikihakikisha wananchi wanapata usafiri salama na huduma
bora katika hospitali hiyo.
Hata hivyo Mhe. Mshagatila ameeleza kuwa, licha ya ukarabati huo wa awali, Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini, Mhe. Paschal Patrobas Katambi, ameahidi kuwa barabara hiyo ya Kolandoto itaboreshwa kwa kiwango cha lami ili kutoa suluhisho la kudumu kwa wananchi.
Diwani Mshagatila amemshukuru Mbunge Katambi na kampuni ya CHICO kwa ushirikiano huo, akisisitiza kwamba hatua kama hizo zinaongeza maendeleo ya miundombinu na kuboresha maisha ya wananchi wa Shinyanga.




Post a Comment