" MHE. BAHATI HENERICO ACHAGULIWA KUWA MWENYEKITI WA ALAT KAGERA.

MHE. BAHATI HENERICO ACHAGULIWA KUWA MWENYEKITI WA ALAT KAGERA.

Na Fabius Clavery, Misalaba Media-Kagera.

‎Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera, Mhe. Bahati Henerico, amechaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) Tawi la Mkoa wa Kagera kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.

‎Mhe. Henerico amepata ushindi huo katika uchaguzi uliofanyika Januari 14 2026,katika Ukumbi wa Manispaa ya Bukoba, baada ya kupata kura 24 dhidi ya kura 8 alizopata mshindani  wake, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba, Mhe. Justus Magongo.

‎Uchaguzi huo ulihudhuriwa na wajumbe wa ALAT kutoka halmashauri zote za mkoa wa Kagera, wakiwemo wenyeviti wa halmashauri pamoja na wakurugenzi watendaji.

‎Akizungumza mara baada ya kuchaguliwa, Mhe. Henerico amewashukuru wajumbe kwa kumuamini na kumpa dhamana hiyo, huku ameahidi kuiongoza ALAT Mkoa wa Kagera kwa misingi ya ushirikiano, uwajibikaji na maslahi mapana ya wananchi wa mkoa huo.

‎Aidha, amewaomba wenyeviti wa halmashauri pamoja na wakurugenzi watendaji kuendelea kushirikiana kwa karibu ili kuimarisha utendaji wa serikali za mitaa na kuhakikisha changamoto zinazowakabili wananchi katika maeneo yao zinapatiwa ufumbuzi wa pamoja kupitia ALAT.






Post a Comment

Previous Post Next Post