" Mke wa Profesa Jay Hakulalamika Licha ya Kupitia Changamoto za Ugonjwa wa Mumewe

Mke wa Profesa Jay Hakulalamika Licha ya Kupitia Changamoto za Ugonjwa wa Mumewe

 

Anachopitia Mkubwa Fella kwa sasa kimenikumbusha hali aliyowahi kupitia Profesa Jay, ambapo aliugua kwa kiwango kikubwa hadi kufikia hatua ya kuzushiwa kifo mara kadhaa. Pamoja na picha zake kuvujishwa mitandaoni akiwa mahututi, mke wake alisimama imara naye, bila kulalamika wala kulaumu ndugu, marafiki au wasanii kwa kutotoa msaada.

Upande wa pili hivi karibuni, mke wa Mkubwa Fella amekuwa akijitokeza mara kwa mara kulalamika na kulaumu watu kwa kutomsaidia mumewe, hatua ambayo kwa wengi hawajafurahishwa nayo, hasa anapotupa lawama kuwa Diamond Platnumz amekata msaada.

Kwa kweli, wanawake wote wanapaswa kuiga hekima na busara ya mke wa Profesa Jay aliyesimama kwa utulivu, upendo na heshima hadi mume wake akapona. Ukomavu kama huu unapaswa kuigwa na kuheshimiwa.

Post a Comment

Previous Post Next Post