
JESHI la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro linafanya uchunguzi wa tukio la kujinyonga kwa mtuhumiwa aitwaye Michael Lambau (18), mkazi wa mtaa wa Karikacha, Kata ya Rau Manispaa ya Moshi akiwa mahabusu katika kituo cha Polisi Moshi Kati.
Kwa mujibu kwa Kamanda Polisi mkoa, SACP Simon Maigwa alisema kuwa, mtuhumiwa huyo alikuwa akishikiliwa kwa kosa la Shambulio la kudhuru mwili.
Alisema kuwa, mtuhumiwa alikamatwa Januari 13, 2026 kwa tuhuma za kumshambulia kwa kumpiga na
mabapa ya panga Brian Felix ambaye ni baba yake mdogo na kujinyonga siku hiyo hiyo.
Aidha, awali alituhumiwa kufanya tukio la mauaji ya baba yake mzazi Novemba 22, 2025 kwa kumchoma na kitu
chenye ncha kali shingoni na alitoroka hadi alipokamatwa kwa tukio hilo la shambulio la kudhuru mwili.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment