
Msemaji Mkuu wa Serikali ya Tanzania, Gerson Msigwa amesema kusitishwa kwa safari za treni kati ya Morogoro na Dodoma hakutokani na kuharibika kwa reli bali ni hatua za kitahadhari ili kudhibiti tishio la mito iloyojaa isiharibu miundombinu hiyo.
Akizungumza na vyombo vya habari leo kwa njia ya simu, Msigwa amesema wakati wowote kuanzia sasa Shirika la Reli Tanzania (TRC) litatangaza kurejea kwa safari za abiria kutoka mikoa hiyo miwili.
Katika hatua nyingine, Msigwa amesema Serikali imeanza utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa Mabwawa sita ya maji katika maeneo hayo ambayo yatatumika kwa shughuli za uvuvi, kilimo sambamba na kukabiriana na maji ya mvua.
“Kama ambavyo TRC ilitoa taarifa safari za treni za SGR kati ya Morogoro na Dodoma zimesitishwa ikiwa ni hatua za kitahadhari na zimechukuliwa kwa sababu mito miwili ambayo inakatiza katika reli yetu ya SGR nikiwa na maana ya Mto Kidete na Msaze katika eneo la Godegode imepata athari kubwa ya mvua zinazoendelea kunyesha maji yamekuwa mengi yanaleta madhara kwenye kingo za mito kumekuwa na mmomonyoko mkubwa,
“Athari hizi zinatishia kuathiri reli yetu ya SGR kwahiyo shirika letu limechukua hatua za kitahadhari sio kwamba reli imeharibika hapana ni hatua za kitahadhari ili maji mengi yaliyojaa katika mito na kuleta tishio la kuathiri treni yaweze kudhibitiwa na kingo za reli zidhibitiwe vizuri na kitu hicho kimesababisha safari za treni zisitishwe wakati hatua hizo za kitahadhari kutokana na athari zilizojitokeza zikichukuliwa,”
“Watanzania wajue kilichofanyika ni kujihadhari, kuilinda reli yetu sasa katika hali ambayo mvua kubwa zinanyesha mito inaleta maji mengi na inaleta athari katika kingo zake huwezi kuruhusu treni iendelee kufanya safari zake kama kawaida kwa sababu hakuna anayejua nguvu hii ya maji italeta athari gani,”.
Watu wamekuwa na hoja kwamba mradi ni mpya kwanini tahadhari hizi hazikuchukuliwa katika upembuzi yakinifu, tahadhari zimechukuliwa na niwaambie tu mradi wetu wa SGR katika kipande cha Dar es Salaam hadi Morogoro, Morogoro hadi Dodoma kipo katika uangalizi chini ya Mkandarasi na anaendelea kufanya jitihada za kuhakikisha analinda miundombinu ya reli,”
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment