" CAF KUVAMIA DAR JANUARY 13! MOTSEPE KUONGOZA MKUTANO MUHIMU WA SOKA AFRIKA

CAF KUVAMIA DAR JANUARY 13! MOTSEPE KUONGOZA MKUTANO MUHIMU WA SOKA AFRIKA

‎Na Mwandishi wetu, Misalaba Media

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), Dkt. Patrice Motsepe, anatarajiwa kuwasili nchini Tanzania kwa ajili ya kuongoza mkutano wa Kamati Tendaji ya CAF utakaofanyika jijini Dar es Salaam Februari 13, 2026.

‎Akizungumza leo Februari 9, 2026, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, amesema maandalizi ya mkutano huo yako katika hatua za mwisho, huku viongozi mbalimbali wa CAF wakianza kuwasili nchini kuanzia leo kwa ajili ya kushiriki mkutano huo muhimu wa soka barani Afrika.

‎Waziri Makonda amesema kuandaliwa kwa mkutano huo nchini Tanzania ni ishara ya imani kubwa ya CAF kwa taifa hili, sambamba na kutambua mchango wake katika kuendeleza michezo, hususan soka, pamoja na kudumisha amani na utulivu.

‎Ameeleza kuwa fursa hiyo ni matokeo ya diplomasia ya michezo iliyoasisiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye ameendelea kuitangaza Tanzania kimataifa kama nchi salama, yenye miundombinu bora na inayofaa kuandaa matukio makubwa ya kikanda na kimataifa.

‎“Mkutano huu ni fursa adhimu kwa Tanzania kukuza soka lake, kuimarisha mahusiano ya kimataifa na kujiweka kwenye ramani ya michezo barani Afrika,” amesema Makonda.

‎Mkutano wa Kamati Tendaji ya CAF unatarajiwa kujadili masuala mbalimbali ya maendeleo ya soka barani Afrika, ikiwa ni pamoja na mipango ya mashindano, uboreshaji wa miundombinu na usimamizi wa soka katika nchi wanachama.

 

Post a Comment

Previous Post Next Post