" JESHI LA POLISI MBEYA LAOMBWA KUSHIRIKIANA KUPAMBANA NA MAWAKILI VISHOKA

JESHI LA POLISI MBEYA LAOMBWA KUSHIRIKIANA KUPAMBANA NA MAWAKILI VISHOKA

Na Lydia Lugakila, Misalaba MediaMbeya Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limeombwa kutoa ushirikiano wa karibu katika kukabiliana na mawakili wanaojiita vishoka, wakati kampeni maalum ya kuwabaini na kuwachukulia hatua itakapoanza.Ombi hilo limetolewa na Mwenyekiti wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Wakili Philip Mwakilima, wakati akihutubia katika maadhimisho ya siku ya Sheria nchini 2026 yaliyofanyika katika viwanja vya mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Mbeya.Mwakilima amesema kuwa TLS inatarajia kuanza kampeni maalum ya kuwaondoa mawakili vishoka pamoja na ofisi hewa, hususan katika maeneo ya wilayani, hivyo ameomba Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa (RPC) kutoa ushirikiano wa kutosha ili kufanikisha zoezi hilo.Ameeleza kuwa ushirikiano wa Jeshi la Polisi utasaidia pindi TLS itakapofanya ziara katika wilaya mbalimbali, ili kuwashughulikia watu wanaojihusisha na shughuli za uwakili bila kuwa na sifa wala usajili halali.Akikiri kuwepo kwa tatizo la mawakili vishoka, Mgeni Rasmi katika maadhimisho hayo, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya, Mhe. Joachim Charles Tiganga, amesema uwepo wa vishoka unaathiri kwa kiasi kikubwa mstakabali wa haki kwa wananchi.Mhe. Jaji Tiganga ameeleza kuwa vishoka hutengeneza nyaraka zisizo halali, ambazo zinapogundulika mahakamani kuwa zimetengenezwa na watu wasio na sifa, hukosa thamani ya kisheria na hivyo kuwanyima wananchi haki zao.“Vishoka ni watu wanaofanya biashara bila kusajiliwa na bila kulipa kodi, na kwa kiasi kikubwa wanaharibu taaluma ya sheria pamoja na biashara ya mawakili halali waliokidhi vigezo vyote,” amesema Mhe. Jaji Tiganga.Aidha, amemuomba Kamanda wa Polisi Mkoa (RPC) kuhakikisha anatoa ushirikiano wa dhati ili kutokomeza kabisa tatizo la mawakili vishoka katika sekta ya sheria.Ukumbukwe kuwa maadhimisho hayo yamebeba kauli mbiu isemayo "mchango wa mahakama katika ustawi wa maendeleo ya Taifa"


 

Post a Comment

Previous Post Next Post