Jumuiya ya Wazazi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mpanda Februari 01, 2026 imefanya maadhimisho ya miaka 49 ya kuzaliwa kwa CCM kwa kufanya shughuli mbalimbali za kijamii na za chama, ikiwa ni sehemu ya kuenzi historia ya chama hicho na kuimarisha ufanisi wa utendaji kazi ngazi ya msingi.
Maadhimisho hayo yamefanyika katika Kata ya Nsemulwa, Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Mjini.
Hafla hiyo imefanyika chini ya uongozi wa CCM Wilaya ya Mpanda, ikiongozwa na Mgeni Rasmi Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mpanda Ndg. Joseph Rwamba pamoja na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda Ndg. Pius Buzumalle.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mgeni Rasmi ameweka wazi kuwa hatua hiyo imelenga kuimarisha utendaji wa kazi katika ngazi ya kata kwa kuhakikisha kata ya Nsemulwa, kituo cha Afya cha Nsemulwa kinakuwa na vifaa vitakavyosaidia utekelezaji wa shughuli za kijamii kwa wakati na kwa ufanisi.
Aidha, Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda imesisitiza umuhimu wa kuendelea kuimarisha ushirikiano kati ya chama na taasisi za elimu, pamoja na kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia katika kituo cha Afya cha Nsemulwa ili kuchangia maendeleo ya sekta ya elimu na afya kwa ujumla.
Katika hafla hiyo, viongozi wamegusia pia masuala ya elimu kwa kuhimiza malezi bora ya watoto kulingana na umri wao, kuhamasisha wananchi kuchukua na kuendeleza masomo, pamoja na kuongeza ushiriki wa wazazi na jamii katika masuala yanayohusu elimu ya watoto.
Kama sehemu ya kuunga mkono juhudi za utunzaji wa mazingira, Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda Ndg. Jimotoli Jilala Maduka pamoja na Mkurugenzi wa Shule ya Sayansi Ndg. Mbosoli, ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ndogo ya Elimu, Malezi na Mazingira katika Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya Wilaya ya Mpanda wameshiriki zoezi la upandaji miti katika Kata ya Nsemulwa ikiwa ni ishara ya kulinda mazingira na kuunga mkono maendeleo endelevu.
Kwa ujumla, Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda imeeleza dhamira yake ya kuendelea kushirikiana na chama pamoja na taasisi mbalimbali ili kuhakikisha maendeleo ya elimu, mazingira na ufanisi wa chama yanaendelea kuimarika kwa manufaa ya wananchi wote.
Mgeni Rasmi, Ndg. Rwamba, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mpanda, amemwakilisha Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Katavi, Ndg. Iddi Hassan Kimanta, katika maadhimisho ya sherehe za miaka 49 ya CCM yaliyofanyika kupitia Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda, Mkoa wa Katavi. Maadhimisho hayo yalifanyika kwa kufariji wagonjwa na kujulia hali zao katika Kituo cha Afya Nsemulwa, pamoja na kushiriki zoezi la upandaji miti katika eneo la kituo hicho cha afya.
Ndg. Rwamba akipanda miti eneo la Kituo cha Afya Nsemulwa.
Ndg. Jimotoli Jilala Maduka, Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda, Mkoa wa Katavi, akishiriki zoezi la kupanda na kumwagilia miti katika maadhimisho ya sherehe za miaka 49 ya CCM yaliyofanyika katika Kituo cha Afya Nsemulwa.
Ndg. Jimotoli Jilala Maduka, Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda, Mkoa wa Katavi, akishiriki zoezi la kupanda na kumwagilia miti katika maadhimisho ya sherehe za miaka 49 ya CCM yaliyofanyika katika Kituo cha Afya Nsemulwa.
Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Nsemulwa, Dkt. Rest, akitoa maelekezo kuhusu matumizi ya vifaa vya upasuaji na namna vinavyofanya kazi.
Ndg. Aziza Said Self ameshiriki maadhimisho ya sherehe za miaka 49 ya CCM Wilaya ya Mpanda, Mkoa wa Katavi, kupitia Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda, kwa kumwakilisha Katibu wa CCM Wilaya ya Mpanda, Ndg. Mussa Ramadan Mwevi. Maadhimisho hayo yalihusisha kufariji wagonjwa na kujulia hali zao katika Kituo cha Afya Nsemulwa, pamoja na kushiriki zoezi la upandaji miti katika eneo la kituo hicho cha afya.
Ndg. Sophia Abdull Hamady, Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Mkoa wa Katavi, ameungana na Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda, Mkoa wa Katavi, kuadhimisha sherehe za miaka 49 ya CCM.
MKURUGENZI wa Shule ya Sayansi, Ndg. Mbosoli, ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Ndogo ya Elimu, Malezi na Mazingira katika Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Mpanda, ameshiriki maadhimisho ya sherehe za miaka 49 ya CCM Wilaya ya Mpanda kwa kupanda miti pamoja na kufariji wagonjwa katika Kituo cha Afya Nsemulwa.🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254


















































Post a Comment