Maafisa usafirishaji maarufu bodaboda wameaswa kuwa makini zaidi katika shughuli zao za kila siku kwa kuepuka kumuamini mtu wasiyemfahamu, hususan pale wanapopewa ofa ya pesa kubwa kutoka kwa wateja wasiowajua. Vilevile wametakiwa kuhakikisha vituo vyao vinatambulika kwa majina rasmi na kutoa taarifa kwa vyombo husika wanapokutana na watu au mazingira yanayowatia shaka.Wito huo umetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Janeth Magomi, wakati akizungumza na waendesha bodaboda katika eneo la Nyamilangano, Halmashauri ya Ushetu. Amesisitiza kuwa ulinzi na usalama ni jukumu la kila mmoja, hivyo ushirikiano kati ya Maafisa hao na Jeshi la Polisi ni muhimu katika kudhibiti uhalifu.Aidha, waendesha bodaboda wametakiwa kuhakikisha wanatafuta na kuwa na leseni halali za udereva pamoja na bima, hatua itakayowasaidia kujilinda wao wenyewe na abiria wao pale ajali au changamoto nyingine zinapojitokeza.🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254



Post a Comment