Zaidi ya kilo 6,750,000 za pamba mbegu zinatarajiwa kuzalishwa katika wilaya za Mbogwe na Bukombe katika msimu wa 2025/2026, kupitia chama kikuu cha ushirika Mbogwe na Bukombe (MBCU).Matarajio hayo yatafikiwa endapo wakulima watachukua na kupanda mbegu zote zilizotolewa, hatua itakayoongeza kipato cha wakulima na kukuza uchumi wa vyama vya ushirika.Akizungumza katika Mkutano Mkuu wa 8 wa MBCU, Mwenyekiti wa chama hicho Said Tangawizi amesema, uzalishaji huo unatarajiwa kupatikana kutoka katika ekari 45,000 zitakazolimwa na wakulima kutoka halmashauri za Mbogwe na Bukombe.Ameeleza kuwa matarajio hayo ni sehemu ya mkakati wa chama wa kuimarisha zao la pamba na kuhakikisha wakulima wananufaika moja kwa moja na juhudi zao za uzalishaji.Amesema katika mwaka wa fedha 2026/2027, chama hicho kinatarajia kununua na kuchambua pamba katika kiwanda cha MBCU LTD kilichopo Masumbwe wilayani Mbogwe, kwa lengo la kuongeza mapato ya chama na wakulima wa pamba. Amapo kwa mujibu wa mpango huo, chama kinatarajia kununua pamba jumla ya kilo 5,000,000 zenye thamani ya shilingi 9,552,979,000 kutoka kwa wakulima wa Mbogwe, Bukombe pamoja na maeneo mengine.Tangawizi amesema chama kinakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo kuchelewa kupatikana kwa mikopo ya kununulia pamba kutoka Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB).“Changamoto ni kuyumba kwa soko la pamba nyuzi na pamba mbegu, pamoja na kupanda kwa gharama za uendeshaji wa zao na uchambuaji wa pamba kunakosababishwa na kupanda kwa bei ya mafuta ya petroli.” Amesema TangawiziAkitaja mafanikio yaliyopatikana katika msimu uliopita, meneja wa MBCU Paul Samwel amesema chama kimefanikiwa kutoa ajira kwa vijana na akina mama katika kipindi chote cha uzalishaji wa pamba, pamoja na kuhakikisha malipo kwa wakulima yanafanyika kwa wakati, jambo lililosaidia kuongeza imani ya wakulima kwa chama hicho.Akizungumza kwenye mkutano huo, mrajisi msaidizi wa vyama vya ushirika mkoa wa Geita Doreen Mwanri amewataka wanaushirika kubadilika kuacahana na kilimo cha mazoea na kulima kisasa ili kupata faida ya kilimo chao.“Baadhi ya wakulima mnaendelea kulima kwa mkono, mnajichosha, mnajikatisha tamaa na kilimo chenu, kwa hiyo nataka kusema hivi, tokeni huko tulime kisayansi tunufaike na kilimo chetu ili tukipende.” Amesema MwanriKatika hatua nyingine amewakumbusha wanaushirika kurejea sheria ya usajili hususani kwenye suala la ununuzi wa hisa ili waendelee kuwa na sifa zilizoainishwa kwenye sheria hiyo.Mkutano huo mkuu wa 8 wa MBCU pia umejadili namna ya kukabiliana na changamoto mbalimbali ikiwemo baadhi ya wajumbe kutonunua hisa, suala la utunzaji wa mazao yao kwa kushirikiana na serikali na wadau wa sekta ya kilimo ili kuendeleza zao la pamba kwa tija na kwa manufaa ya wakulima.Mwisho.

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254




Post a Comment