" MWENYE ULEMAVU AKABIDHIWA NYUMBA KYERWA

MWENYE ULEMAVU AKABIDHIWA NYUMBA KYERWA

‎Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa , Mhe.Zaituni Msofe, amekabidhi nyumba kwa familia ya mlemavu, Ndg Jenifer Richard, mkazi wa Kakerere Kata ya Nkwenda, iliyojengwa na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kagera, Mhe.Devotha Daniel Mburarugaba, kama msaada wa kuwapunguzia changamoto za makazi.

‎Akizungumza wakati wa makabidhiano, Msofe amempongeza mbunge huyo kwa kuonyesha mfano wa kusaidia wananchi wenye uhitaji maalum na kuhimiza jamii kuendelea kusaidiana.

‎Mbunge Mburarugaba amesema aliguswa kujenga nyumba hiyo baada ya kuona hali ya maisha ya familia hiyo kupitia mitandao ya kijamii, na amethibitisha pia atagharamia bima ya afya kwa familia hiyo ili waweze kupata huduma za matibabu kwa uhakika.

‎“Nilipoona hali aliyokuwa nayo, niliguswa kuchukua hatua ya haraka. Leo tunashuhudia matokeo ya mshikamano na upendo,” amesema Mbunge huyo


‎Mbunge huyo pia amemshukuru Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira yanayowezesha viongozi kuwahudumia wananchi.

‎Familia hiyo imeishukuru serikali, mbunge na wadau wote kwa msaada huo uliorejesha matumaini mapya ya maisha.






 

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254



Post a Comment

Previous Post Next Post