" NKWERA ATHIBITISHA HATUA YA MWISHO YA MRADI WA MTO KANONI

NKWERA ATHIBITISHA HATUA YA MWISHO YA MRADI WA MTO KANONI


Lydia Lugakila, Misalaba MediaBukobaMkurugenzi wa Manispaa ya Bukoba, Jacob Nkwera, ametangaza kuwa utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa kingo za Mto Kanoni unatarajiwa kuanza rasmi Febuari 28, 2026, baada ya kukamilika kwa taratibu za kumpata mkandarasi mshauri.Nkwera alitoa taarifa hiyo wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika  Februari 9 katika ukumbi wa Manispaa ya Bukoba, akijibu swali la Diwani wa Kata ya Bilele, Taufiq Sharifu, aliyehoji ucheleweshaji wa kuanza kwa mradi huo licha ya mkandarasi kutambulishwa na mkataba kusainiwa zaidi ya miezi sita iliyopita.Akizungumza mbele ya baraza hilo, Nkwera alisema kuwa hatua muhimu ya awali ya kumpata mshauri wa mradi tayari imekamilika, na kinachosalia ni kuanza kwa utekelezaji wa moja kwa moja wa kazi.“Tarati​bu zote za kumpata mshauri zimekamilika tunatarajia ujenzi wa kingo za Mto Kanoni kuanza rasmi tarehe 28 Februari,” alisema Nkwera.Kwa upande wake, Diwani Taufiq Sharifu alisema ucheleweshaji wa mradi huo unaendelea kuwa chanzo cha wasiwasi kwa wananchi wanaoishi kandokando ya Mto Kanoni, hasa kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha na kusababisha mafuriko ya mara kwa mara.“Wananchi wanaishi kwa hofu kubwa mvua za hivi karibuni tayari zimeshaanza kuleta mafuriko hivyo sisi kama madiwani tunapata presha kubwa kutoka kwa wananchi wetu,” alisema Sharifu, akisisitiza haja ya mradi kuanza mara moja.Naye Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Bukoba Mjini, Shabani Mdoe, alisema chama hicho hakijaridhishwa na kasi ya utekelezaji wa mradi huo, akieleza kuwa ni miongoni mwa miradi mikubwa inayobeba matumaini ya wananchi wa Bukoba Mjini.Aliongeza kuwa mradi huo ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2025–2030, hivyo ni wajibu wa serikali kuhakikisha unaanza na kukamilika kwa wakati.“Huu ni mradi wa kugusa maisha ya wananchi moja kwa moja kwa moja miezi sita bila utekelezaji ni muda mrefu sana,” alisema Mdoe.Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Erasto Sima, alisema serikali itaendelea kuusimamia mradi huo kwa karibu ili kuhakikisha unaanza kwa wakati uliopangwa, akibainisha kuwa mvua za masika huanzia Februari hadi Julai na zimekuwa zikisababisha madhara makubwa kwa wakazi wa maeneo ya jirani na mto huo.Mradi wa ujenzi wa kingo za Mto Kanoni ni sehemu ya miradi ya TACTICS inayotekelezwa katika Manispaa ya Bukoba. Mbali na kudhibiti mafuriko, mkandarasi huyo anatarajiwa pia kujenga barabara za kiwango cha lami zenye urefu wa kilomita 10 pamoja na kufunga taa za Barabarani.

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254


Post a Comment

Previous Post Next Post